RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Thursday, May 31, 2018

MPINA AFUNGUA MAONESHO YA WIKI YA MAZIWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhanga Mpina (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua wiki ya maziwa Kitaifa kwenye uwanja wa maonyesho ya Kilimo na  Mifugo Nanenane Njiro,kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na viongozi wa Baraza la Kilimo na Bodi ya Maziwa.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhanga Mpina akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa wiki ya Maziwa Kitaifa kwenye uwanja wa maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro jijini Arusha.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi mheshimiwa Luhanga Mpina, ameiagiza bodi ya maziwa kwa kushirikiana na baraza la kilimo Tanzania kuandaa maonyesho ya kimataifa ya wiki ya maziwa badala kila mwaka kuadhimisha yakitaifa tu.
Ameyasema hayo alipokuwa akufungua maonyesho ya 21 ya wiki ya maziwa kitaifa, yaliyofanyika katika viwanja vya Themi Njiro jijini Arusha.
Amewataka kuendelea kusimamia sheria na kanuna za maziwa zinazotumika katika kila nchi, kwani soko la maziwa linapanuka kwa kasi sana.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali inaendelea kuhakikisha inabadilisha sheria na kanuni ambazo zinaonekana hazina tija katika sekta hiyo, hii itasaidia sana katika uboreshaji wa soko la maziwa ndani na nje ya nchi.
Amewahasa wafugaji waendelee kutumia ufugaji wa kisasa kwani utaongeza uzalishaji wa maziwa kwa wingi nakutoa fursa zaidi za masoko kwa nchi za nje.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Arusha ameipongeza sana bodi ya maziwa kwa kufanikisha madhimisho hayo ya wiki ya maziwa na amewataka wazalishaji wazingatie zaidi sheria na kanuni za ndani na nje ya nchi ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima.
Magreti Kihumbuli mwakilishi kutoka bodi ya maziwa Kenya, ameishukuru bodi ya maziwa Tanzania kwa kuwapa mwaliko wakushiriki maonyesho hayo.
Amesema anatagemea kujifunza mambo mengi katika maonyesho hayo na hata pia waonyeshaji wa Tanzania watajifunza mengi kutoka kwao na hii itasaidia kuongeza uhusiano bora kati ya nchi hizi.
Luge Kawaga ni mwakilishi kutoka mamlaka ya endelezaji wa maziwa nchini Uganda, amesema maonyesho hayo yatasaidia kubadilisha elimu baina ya nchi hizo tatu.
Maonyesho ya wiki ya maziwa kitaifa yanafanyika mkoani Arusha kwa siku 3 ambapo makapuni takribani 40 yakiwemo ya kigeni yameweza kushiriki maonyesho hayo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina akiwapa wanafunzi wa Shule ya Msingi Baraa ya Jijini Arusha baada ya kuzinduawiki ya Maziwa Kitaifa kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro,kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.


Meneja wa Kampuni ya Milkcom maarufu Dar Fresh,Tunnu Mssika akimpa maelezo Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati akikagua mabanda ya waoneshaji bidhaa mbalimbali zinazotokana na Mifugo.








Wednesday, May 16, 2018

VITUO VYA AFYA KUJENGWA LONGIDO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mbunge wa jimbo la Longido Dkt. Steven Kiruswa, wakishirikiana na wananchi wa kata ya Ketumbeini kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata hiyo,wilayani Longido.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema wananchi wa kata ya Kimokouwa na Namanga kwa ujumla hawana haja yakupata matibabu tena kutoka nchi jirani ya Kenya.
Aliyasema hayo alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha Eworendeke katika kata ya Kimokouwa wilayani Longido.
Gambo amesema kwa mda mrefu sana wananchi wa Namanga kwa ujumla walikuwa wanapata hadha yakufuata huduma ya matibabu Longido mjini au nchi jirani ya Kenya na hivyo kufanya wagonjwa wengi kutembea umbali mrefu.
Amesema kituo hicho cha afya kimepata mgao wa shilingi milioni 700 kutoka serikalini na wananchi wanachangia nguvu kazi katika kukijenga na mpaka sasa kiasi cha milioni 400 ndio kimeshatumika na ujenzi unaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikagua ujenzi wa kituo cha afya cha Engarenabor kitakacho gharimu kiasi cha milioni 200 mpaka kukamilika.

Gambo amesema mbali na serikali kutoa kiasi hicho cha fedha bado bajeti ya ununuzi wa madawa umeongezwa kutoka bilioni 31 hadi bilioni 269 kwa mwaka huu wa fedha, na hii itasaidia huduma ya madawa kupatikana kiurahisi katika kila kituo cha afya na hospitali zote nchini.
Kituo cha afya cha Eworendeke kinatarajia kukamilika Agosti 2018 na huduma zote zitapatikana zikiwemo huduma za  upasuaji na x-ray, hivyo itarahisisha matibabu kwa wananchi wote wa Namanga.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo,amesema asilimia 27 ya wajawazito walikuwa wanajifungulia katika vituo vya afya kwa wilaya nzima na idadi imeongezeka kufikia asilimia 35.
Chongolo amesema ongezeko hili litasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto katika wilaya yake.

Ujenzi wa kituo cha afya cha Eworendeke Namanga unaondelea na kituo kitagharimu kiasi cha milioni 700 fedha kutoka serikalini,kituo kipo wilayani Longido.

Mgaga mkuu wa Mkoa Dokta Vivian Wonanji,amesema serikali imeshatenga kiasi cha fedha cha milioni 200 kwa ajili ya manunuzi ya vifaa kwa vituo vyote vya afya na hospitali kwa mkoa mzima na anaendelea na zoezi la kuongeza watumishi katika sekta ya afya.
Amesema agizo la serikali ni kuhakikisha vituo vyote vya afya vinakuwa na huduma ya x-ray, hivyo katika kituo hicho wanajenga chumba maalumu kitakachotoa huduma hiyo kwa wananchi wote wa Namanga.
Akitoa shukurani zake za dhati kwa serikali bwana Hassan Hamis ambae ni mkazi wa Namanga amesema kweli kituo hicho cha afya kitasadia kuondokana na hadha waliyokuwa wanaipata kufuata matibabu kwa umbali mrefu, na pia itapunguza vifo vilivyokuwa vinatokana na umbali huo.
Gambo anaendelea na ziara yake katika wilaya ya Longido ambapo ametembelea kituo kingine cha afya cha  Engarenaibor kilichogharimu kiasi cha milioni 200, pia ameshiriki ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Ketumbeine.

Monday, May 14, 2018

LONGIDO YAPATIWA SIKU 7 KUJIBU HOJA ZA CAG

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, akisoma baadhi ya hoja zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) katika kikao chake na watumishi wa halmashauri ya Longido.

Halmashauri ya Wilaya ya Longido imepewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) kwa mwaka fedha kuanzia 2015 hadi 2017.
Akitoa agizo hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amesema halmashauri kupata hati ya mashaka kwa hoja zinazojibika na zinazojirudia kila mwaka ni uzembe wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.
“Watumishi bado wapo wachache wanaofanya kazi  kwa mazoea bila ya kufuata sheria na taratibu za kiutumishi”.
Ameuwagiza uongozi wa halmashauri ya Longido kutoa barua za onyo kwa watumishi wote waliotajwa kwenye taarifa ya mkaguzi wa nje ili iwe fundisho kwa watumishi wote umma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,amesema ifike wakati sasa viongozi kutoonea huruma mtumishi yoyote anaebainika ana makosa, kwani hoja nyingi katika halmashuri hiyo zimekuwa zikijirudiarudia kila mwaka.
Amesema  hatua madhubuti ni lazima sasa zichukuliwe ili kudhibiti tabia hii ya mazoea ya hoja kujirudiarudia kila mala.
Akisisitiza zaidi mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo amesema kazi ya viongozi ni kusimamia sheria na taratibu za kazi,hivyo ataendelea kusimamia  sheria za utumishi wa umma katika halmshauri yake kwani mpaka sasa hali imeanza kubadilika kwa watumishi kuwa na nidhani.
Aidha, amesema halmshauri ipo tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa mkoa na kuhakikisha halmashauri yake haitapata tena hati ya mashaka kwa miaka inayokuja.
Gambo yupo katika ziara ya siku 3 wilayani Longido ambapo atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa katika wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo akimchukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada ya kutoa maelekezo ya namna ya kujibu hoja za CAG.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Longido alipokuwa akuzungumzia hoja za CAG.