Viongozi wa Wilaya wa Mkoa wa Arusha wametakiwa
kusimamia kikamilifu zoezi la utoaji dawa za ugonjwa wa vikope (Trakoma) kwenye
maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha ugonjwa huu unatokomezwa kabisa.
Akitoa rai hiyo alipokuwa akifungua semina ya mpango wa kudhibiti
magonjwa yasiyopewa kipaombele kwa niaba
ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, katibu tawala wa mkoa Richard Kwitega
amesema ni vizuri viongozi wakajikita kwa nguvu zote katika zoezi hili
lakutokomeza ugonjwa wa vikope kwenye maeneo yao.
“Ni rai yangu kwenu viongozi wote wa Wilaya na
halmashauri kuhakikisha mnasimamia vyema zoezi hili lakutokomeza ugonjwa huu wa
vikope katika maeneo yenu”.
Lengo la serikali nikutumia rasilimali chache kuthibiti
magonjwa haya ambayo yanaonekana hayapewi kipaombele katika jamii yetu hivyo
kila halmshauri ihakikishe inatenga fedha zakutosha zakusaidia upasuaji wa
vikope.
Wilaya ya Karatu na halmashauri ya Arusha zimejitaidi
kuhakikisha zimetokomeza ugonjwa wa vikope lakini bado katika halmashauri ya
wilaya ya Longido na Ngorongoro, nguvu zaidi zinaitajika katika maeneo haya.
Kwa mkoa wa Arusha watu takribani 1076 wameshafanyiwa
upasuaji wa vikope katika halmshauri zote za wilaya na magonjwa yanayoongoza
katika mkoa huu ni ugonjwa wa Kichocho ,Minyoo ya Tumbo na vikope.
Amewataka washiriki wa semina hiyo kuhakikisha kuwa
elimu wanayoipata katika mafunzo hayo wakaitumie vizuri katika kutokomeza
magonjwa hayo kwenye maeneo yao.
Nae mratibu wa magonjwa yalisiyopewa kipaombele kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii,jinsia,
wazee na watoto Dokta Upendo Mwingira, amesema takribani magonjwa 17 yasiyopewa
kipaombele yapo katika bara la Asia, Amerika ya Kusini na Kusini mwa jangwa la
Sahara.
Amesema magonjwa mengine ambayo hayapewi kipaombele ni
AIDS, TB, Malaria, Kuumwa na nyoka,Matende, Mabusha, Usubi na Ukoma.
Amezitaja athari mbalimbali zinazotokana na magonjwa
haya ni kama mgonjwa kupata ulemavu wa mda mrefu, Udumavu kwa watoto,kupunguza
uwezo wa kufanya kazi,unyanyapaaji, kansa ya kibofu cha mkojo, upofu na presha
ya ini.
Akitoa taarifa fupi ya ugonjwa wa vikope kwa mkoa wa
Arusha Dokta Mwanahawa Kombo kutoka hospitali ya Mkoa Mt. Meru, amesema jumla
ya wagonjwa 1076 wameshapasuliwa vikope na halmashauri ya Monduli imefanya
vizuri katika kukabiliana na ugonjwa huu kati ya halmashauri 2 za Longido na
Ngorongoro.
Semina hii hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa elimu
na takwimu sahihi za hali halisi ya
magonjwa yasiyopewa kipaombele nchini.
Semina hii hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutoa elimu na takwimu
sahihi za hali halisi ya magonjwa
yasiyopewa kipaombele nchini