|
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo (wa katikati) akiwa na Katibu Tawala Msaidizi Elimu Bwana Gift Kyando wakimsikiliza mwalimu Mary Marimo akifafanua namna wanavyowafundisha watoto alama za barabarani katika halmashauri ya Monduli.
|
Viongozi wa Kata wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha
watakiwa kutafuta suluhu ya tatizo la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari.
Akitoa maagizo hayo kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Arusha,mkuu
wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo katika kuhadhimisha siku ya kilele cha
wiki ya elimu Mkoani Arusha.
Amesema changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya elimu
Mkoani Arusha ni mimba kwa wanafunzi hasa wa Sekondari,ambapo kwa mwaka 2017
wanafunzi 237 waligundulika kuwa na ujauzito ikiwa wanafunzi 50 ni wa shule za
Msingi na 187 ni wa Sekondari.
Aidha,kuanzia Januari hadi Aprili 2018 jumla ya
wanafunzi 97 waligundulika kuwa na ujauzito ambapo wanafunzi 17 niwa shule za
Msingi na 80 wa Sekondari.
“Bado tatizo la ujauzito kwa wanafunzi wa kike ni
changamoto kubwa hasa wa sekondari,wazazi bado mna jukumu kubwa hasa la
kuhakikisha mnasimamia maadili ya watoto wenu na pia kuchangia fedha za chakula
mashuleni ilikupunguza vishawishi kwa wanafunzi hawa”.
|
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo akiwa na Katibu Tawala Msaidizi Elimu Gift Kyando na Katibu Tawala wilaya ya Karatu Abas Kayanda wakipata maelekezo ya elimu vitendo kutoka kwa mwanafunzi Omary Ally wa shule ya Mwalimu Anna iliyopo wilayani Monduli .
|
Katibu Tawala msaidizi upande wa elimu bwana Gift
Kyando,amesema changamoto nyingine iliyopo katika sekta ya elimu Mkoani Arusha
ni baadhi ya watoto kutojua kusoma,kuhesabu na kuandika (KKK), kwa sababu
watoto hao hawapatiwi elimu ya awali kwanza kabla ya kujiunga na elimu ya
msingi.
Amesema mbali na changamoto hizo,elimu bure kwa Mkoa wa
Arusha imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya uwandikishaji wa
watoto darasa la kwanza.
Akisisitiza zaidi anasema mradi wa mpango wa kusaidia
kusoma,kuandika na kuhesabu (LANES) umeweza kusaidia sekta ya elimu kwa kiasi
kikubwa kwani mradi umeweza kuongeza Vitabu,Vifaa vya kufundishia na Vyombo vya
usafiri,ambapo kila halmashauri itapatiwa kopyuta 3 za kusaidia utunzaji wa
taarifa mbalimbali za wanafunzi.
|
Mkuu waWilaya ya Karatu Theresia Mahongo akimkabidhi mkuu wa shule ya Bwawani mwl. Revocatus Mmary Kopyuta zilitolewa kutoka kwenye mradi wa LENSI.
Juhudi kubwa inaitajika katika kutoa kipaombele kwa watoto
wenye ulemavu, kwani Mkoa unajumla ya watoto wenye ulemavu 614 ambao wanaitaji
kuwa na madarasa maalumu lakini pia bado kuna baadhi ya wazazi wanawaficha
watoto hao manyumbani.
Bwana John Isiriri ni mmoja wa wazazi waliohudhuria
kilele cha wiki ya elimu,amesema ni kweli kuna tatizo kwa watoto wenye ulemavu
kwa kutopewa kipaombale tokea katika ngazi ya familia zao na hivyo kupelekea
wengi wao kukosa elimu.
Pia amesema tatizo la ujauzito kwa watoto wa kike bado
ni changamoto kwa watoto wao hasa wa sekondari, lakini wazazi sasa wanatakiwa kusimamia
maadili ya watoto wao na pia kuchangia chakula mashuleni ili kupunguza
vishawishi kwa watoto wa kike.
Maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu hufanyika kila
mwaka na mwaka huu 2018 kimkoa yamefanyika katika wilaya ya Karatu kwa lengo la
kuhamasisha utoaji wa elimu bora kwa shule za mkoa wa Arusha.
|