RC Akiapishwa
Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.
Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.
JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja
Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha
Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Picha ya Pamoja
Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Monday, April 10, 2017
Saturday, March 25, 2017
SIKU YA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU.
![]() |
| Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maadhimisho ya siku yakudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu. |
Waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoo,Ummy
Mwalimu amezindua mashine zakisasa (molekyula) zakupima ugonjwa wa kifua kikuu
ambazo zitatumika katika hospitali zote za rufaa nchini na ikiwa ni siku yakudhibiti
ugonjwa wa kifua kikuu duniani.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Arusha nakusisitiza kuwa mashine hizo zinauwezo wakupima wagonjwa 12 kwa siku na zinauwezo
wakugundua usugu wa dawa aliyonao mgonjwa nakupima virusi vya UKIMWI.
Changamoto kubwa ambayo wizara ilikuwa inapata
nikuwagundua wagonjwa wa kifua kikuu mapema nahii imetokana na wagonjwa wengi
kuwa na usugu wa dawa walizokuwa wakitumia na hivyo kuwafanya wasipone kwa
wakati.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la afya dunia Tanzania
inawagonjwa takribani 1060 wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka na
asilimia 30 kati ya wagonjwa 100 tu ndio wanaofika katika vituo vyakupatiwa
tiba.
Mkoa wa Dar es Salaama ndio unaongoza kuwa na wagonjwa
wengi wa kifua kikuu takribani asilimia 22 ikifuatiwa na mikoa ya Mwanza,Mbeya,Morogoro,Shinyanga,Arusha,Mara,Manyara,Tanga
na Kilimanjaro ambayo yenyewe inachangia asilimia 63 ya wagonjwa wote kwa
wagonjwa waliogundulika mwaka 2015.
Mpaka sasa wizara imenunua mashine 70 ambazo wanatarajia
kuzisambaza katika hospitali zote za rufaa za mikoa ikiwa ni awamu ya kwanza na
pia wanampango wakuongeza mashine hizo hadi kufikia 150 ili waweze kubaini
wagonjwa wengi zaidi na hata wale wenye kifua kikuu sugu.
Amesema kutokana na taarifa ya shirika la afya duniani
ya mwaka 2016 Tanzania kila mwaka inashindwa kuwafikia wagonjwa takribani 2400
wenye kifua kikuu sugu na laki moja wenye kifua kikuu.
Hivyo amezitaka halmashauri kuweka mikakati yakubaini
wagonjwa wote wa kifua kikuu kwa kuhakikisha kuwa pindi mgonjwa anapoletwa
hospitali halmashauri ifikie ile kaya ambayo mgonjwa umetoka ili kuwapima
wakazi wote wa kaya hiyo kama kuna ambae ameambukizwa.
Pia amepiga marufuku kwa shule zote za bweni kupokea
mwanafunzi yoyote bila kuwa na fomu maalumu yakutoka hospitali inayoonyesha
vipimo vya magonjwa mbalimbali ambayo mwanafunzi huyo amepimwa ikiwemo ugonjwa
wa kifua kikuu.
Aidha ameagiza wagonjwa wote waliopo kwenye kundi
hatarishi hasa wenye virusi vya UKIMWI, watoto walio chini ya amri wa miaka 5,wamama
wajawazito,wazee,wafungwa, watumiaji wa madawa ya kulevya,watu wenye kisukari
na saratani ni lazima wachunguzwe ugonjwa wa kifua kikuu mara tu wanapofika
kwenye vituo vya tiba.
Pia kundi linguine litakalopimwa ugonjwa huu ni wagonjwa
wanaofika katika idara za nje,cliniki za watu wenye virusi vya UKIMWI na
wagonjwa wote watakaokuwa wamelazwa kwenye hospitali za serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo nae amemwahidi
Waziri Ummy kuongeza ushirikiano katika kupambana dhidi ya ugonjwa huu wa kifua
kikuu kwa kushirikiana na wilaya zote za mkoa kuhakikisha kuwa kila kijiji na mtaa
kwenye mikutano yao mikuu ya hadhara watoe elimu ya kutosha na kuhamasisha
wananchi wakapime afya zao kwenye vituo vya afya.
Wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto
kila mwaka imekuwa ikiadhimisha siku ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu na
mwaka huu siku hiyo ameadhimisha rasmi mkoani Arusha.
Kamati iliyokuwa ikishughulikia mgogoro wa pori tengefu Loliondo imemaliza kazi yake.
WANANCHI
wa Kata Saba Wilayani Ngorongoro ambao wamekubaliana kwa pamoja kwenye
mapendekezo yao juu ya kufikia muafaka wa mgogoro wa eneo la Pori Tengefu la
Loliondo lenye kilomita 1,500 za mraba
wamesema kuwa endapo maoni yao yatakubaliwa na Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa watakuwa na nidhamu juu ya matumizi bora ya ardhi.
wamesema kuwa endapo maoni yao yatakubaliwa na Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa watakuwa na nidhamu juu ya matumizi bora ya ardhi.
Wakizungumza
jana Wilayani hapo wakati wa kikao cha pamoja juu ya
kukubaliana kama eneo hilo la Pori Tengefu Loliondo liwe chini ya
Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori za Jamii (WMA) au Pori Tengefu (GCA) kwaajili ya wanyama pekee ,wananchi hao walipendekeza kwa pamoja kuwa eneo hilo ni vyema likawa WMA ili jamii iweze kunufaika na maliasili zilizopo.
Wakizungumza
jana mbele ya Kamati ya Utatuzi wa Mgogoro huo wa matumzi ya Ardhi ya Pori
Tengefu la Loliondo, ambayo inaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
wanachi hao walisema ni bora Pori hilo likawa chini ya WMA ili vijiji
vinavyozunguuka kata hizo viweze kunufaika na mapato yanayotokana na utalii.kukubaliana kama eneo hilo la Pori Tengefu Loliondo liwe chini ya
Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori za Jamii (WMA) au Pori Tengefu (GCA) kwaajili ya wanyama pekee ,wananchi hao walipendekeza kwa pamoja kuwa eneo hilo ni vyema likawa WMA ili jamii iweze kunufaika na maliasili zilizopo.
Lakini wengine wakiongozwa na Yanick Ndoinyo walionyesha hofu ya kuwa
na WMA kwa madai kuwa mapato ya kijiji kimoja hivi sasa yatakwenda
kwavijiji vyote vilivyopo kwenye kata saba zilizohusishwa na mgogoro
huo.
“Yani hapa tunatatua mgogoro lakini tunatengeneza mgogoro mwingine
maana ni lazima vijiji vipimwe na tukubaliane kuwa wamoja na kugawana
fedha hofu yangu ni kuwa je vile vijiji vinavyopata hela hapo awali na
hazijulikani zinakwenda wapi vitakubali”.
Alisema
ngoja tuone maana tuliyokubali ni sisi kutoa mapendekezo haya
na endapo yatakubaliwa na Waziri Mkuu, Majaliwa hii itatutafuna
wenyewe kwa wenyewe maana hii ngoma bado nzito lakini tunamshukuru Rc Gambo kwa uamuzi huu ila ni lazima tukubaliane juu ya suala hili.
Lakini hoja
za kuwa WMA zilipingwa kitaalam na wahifadhi kutokana endapo yatakubaliwa na Waziri Mkuu, Majaliwa hii itatutafuna
wenyewe kwa wenyewe maana hii ngoma bado nzito lakini tunamshukuru Rc Gambo kwa uamuzi huu ila ni lazima tukubaliane juu ya suala hili.
Hifadhi mbalimbali za Taifa,ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori,
Profesa ,Alexander Songorwa alisema kuwa haiezekani mtoto akawa na
mama wawili huku akimaanisha kuwa sheria za wanyamapori na sheria ya
WMA zinakinzana.
“Ili
pori hili liweze kuendelea ni lazima kuhakikisha Ikolojia hii
inahifadhiwa kwaajili ya kulisha Hifadhi ya Serengeti pamoja na eneo
hilo la Pori Tengefu kuwa la mazalia ya wanyama hivyo eneo hilo endapo
litaenda WMA hifadhi hii ya Serengeti itakufa”.
Alisema
lakini haya ni mapendekezo tu yanaweza yakakubaliwa au lainahifadhiwa kwaajili ya kulisha Hifadhi ya Serengeti pamoja na eneo
hilo la Pori Tengefu kuwa la mazalia ya wanyama hivyo eneo hilo endapo
litaenda WMA hifadhi hii ya Serengeti itakufa”.
hivyo kila mtu amesema analitaka kwaajili gani na mwisho wa siku
Waziri Mkuu,Majaliwa atapokea mapendekezo hayo na kasha kutolewa
maamuzi.
Kamati hiyo iiliyoongozwa na Rc Gambo ilikuwa Wilayani Ngorongoro
tangu Machi 15 hadi Machi 21 mwaka huu huku ikikumbana na manadamano ya mara kwa mara kwa wananchi lakini pia wajumbe hao wa kamati walaifanya kazi usiku kucha kushughulikia mgogoro huo kwa kukusanya maoni ya wafugaji,wahifadhi pamoja na wataalam wa ardhi na hatimaye wannachi walitoka na mapendekezo ya kukubali eneo hilo kuwa WMA.
Wanawake wapigwa marufuku kushinikizwa kuandamana.
| Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Loliondo wakiandamana kupinga kamati wa utatuzi wa mgogoro wa pori tengefu. |
BAADHI ya Wanawake pamoja na watoto wanatumiwa kama chambo kwaajili ya kusimamisha msafara wa Kamati ya Kukamilisha mchakato wa Utatuzi wa Mgogoro wa Matumizi ya Ardhi kwenye Pori Tengefu la Loliondo.
Kutumika kwa wanawake hao ambao baadhi yao walikuwa na watoto wadogo migongoni kumebainika jana wakati kamati hiyo ilipokuwa ikiendelea kuangalia maeneo mbalimbali ya Pori hilo Tengefu la Loliondo lenye ukubwa wa kilomita 15,000 za mraba zilizoleta mgogoro kwa zaidi ya miaka 25 sasa.
Wanawake hao katika Kata ya Malambo na Kata ya Arash,ambao kwa pamoja walibeba mabango ya kuisihi Kamati hiyo kutenda haki mengine
yakimtuhumu Waziri wa Maliaisili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe
wakidai kuwapenda wanyamapori kuliko binadamu.
Baadhi ya wanwake hao ambao ni Rehema Pascal na Lemnyaki John
walisimamisha mafara huo kwakuonyesha mabango yao yanayodai kutokubali kuhamishwa katika Pori hilo huku wengine wakipandisha mori na kupiga mayowe.
Baada
ya Rc,Gambo kuyasoma mabango hayo aliwapa vipaza sauti ili
wayasome tena hapo ndipo waliposhindwa kuyasoma na kudai kuwa hawajui Kiswahili.
wayasome tena hapo ndipo waliposhindwa kuyasoma na kudai kuwa hawajui Kiswahili.
“Nani
aliyewaandikia mabango haya wakati hamjui kusoma ,mnatumiwa na
viongozi wenu hukusu mgogoro huu ,msikubali kutumika maana hamjui
serikali inafanya hivi kwa nia ipi na wala serikali haina mpango wa
kuchukua ardhi hii bali tunachokifanya ni kujua hayo mnayoyasema yapo
kiuhalisia au la ili tukamilishe kazi yetu”.
Naye Makamu
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Felex Wandwe alisisitizaviongozi wenu hukusu mgogoro huu ,msikubali kutumika maana hamjui
serikali inafanya hivi kwa nia ipi na wala serikali haina mpango wa
kuchukua ardhi hii bali tunachokifanya ni kujua hayo mnayoyasema yapo
kiuhalisia au la ili tukamilishe kazi yetu”.
aliwatoa hofu wananchi wa Kata saba za wilaya hiyo kutokubali kutumika
vibaya kwaajili ya Pori hilo kwani serikali inachofanya hivi sasa ni
kuchukua mapendekezo ya kamati hiyo kisha kuyawasilisha kwa Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa .
“Msikubali
kutumiwa kwa maslahi ya wengine sisi tupo pamoja na
wawakilishi wenu na kabla ya kuanza zoezi hili walijua tunakuja
kufanya nini hivyo mtulie”.
Pia Katibu
wa Kamati hiyo, Bahati Chisanza alisema kuwa ni vyemawawakilishi wenu na kabla ya kuanza zoezi hili walijua tunakuja
kufanya nini hivyo mtulie”.
wananchi wakajua kuwa serikali haichukui ardhi bali inachokifanya ni
kutaka kupanga matumzii bora ya ardhi ili kila mtu anufaike nayo.
Awali Mwenyekiti wa Kijiji cha Malambo, Lazaro Mashele alitoa rai kwa
kamati hiyo kutoiingiza Kata hiyo ya Malambo katika matumizi bora ya
ardhi kwani kata hiyo haina mgogoro na Pori hilo bali ni wahifadhi
wazuri wa wanyamapori ingawa kata hiyo ni sehemu ya mazalia ya
wanyama.
“Tunawaomba wakuu kata hii isiingizwe katika mgogoro huu kwani hatupo
ndani ya vijiji saba lakini pia kata hii inatumika kwaajili ya mazalia
ya wanyamapori ambao hatuna ugomvi nao”.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo alisisitiza kuwa wamechukua maoni ya mwenyekiti huyo na watafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa na
wananchi hao ,wahifadhi na wataalam wa ardhi kisha kuyawasilisha kwa
Waziri Mkuu Machi 25 mwaka huu.
Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo
alitoa rai kwa wananchi hao kutokubali kutumika kwa msalahi ya
wengine na kutoa rai kwa viongozi wa vijiji,madiwani na mashirika
yasiyo ya kiserikali kuacha mara moja kuwatumia wananchi kwaajili ya
kuwapotosha kuhusu Pori Tengefu la Loliondo.
Pia alisema polisi wataanza msako kwa wale wote ambao si raia wa
Tanzania wanaoishi Wilayani Loliondo huku akisisitiza kuwa wamemkamata
mtu mmoja ambaye ni mwanaume (hakumtaja jina) kwa kufanya vurugu
wakati kamati hiyo ilipokuwa ikifanya kazi yake katika kata mbalimbali
na muda wowote atafikishwa mahakamani wilayani humo.
Saturday, February 18, 2017
VIJANA JIJINI ARUSHA WAPEWA SIRI YA MAFANIKIO YAO.
| Mkuu wa wilayaya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro akizungumza na baadhi ya vijana wa jiji la Arusha wakati akifungua mdahalo wa vijana kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. |
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro
amefungua mdahalo wa vijana wa jijini Arusha kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo, uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha(ATC),mdahalo ulikuwa na
lengo lakutoa elimu kwa vijana juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo
katika Mkoa wa Arusha.
Daqarro aliwahamasisha vijana kujiunga na vikundi
mbalimbali vilivyosajiriwa ili waweze kupata mikopo ya serikali itakayowasaida
katika shughuli mbalimbali zakuinua uchumi wao badala ya wao kukaa vijiweni
nakulalamika hakuna ajira.
“Ni vema vijana mkajiunga kwenye vikundi vya watu 8 hadi
30 na mkavisajiri ili muweze kupata mikopo kutoka serikalini kuliko kukaa
vijiweni nakusubiri ajila ziwafuate au kulalamika hakuna ajira”.
lisisitiza kuwa vijana pia watafute fursa kwenye soko
la jumuiya ya afrika masharika kwani wakilala wao ndio watageuzwa kuwa soko
kwasababu fursa zote zitachukuliwa na wageni.
Pia amewahasa wasipendi urahisi wamaisha kwakutaka
mafanikio haraka kwa njia zisizo halali kwani ndio zinawapelekea wajiingize
katika biashara harama kama zakuuza na kutumia madawa ya kulevya.
Hata hivyo taasisi mbalimbali nazo ziliweza kuonyesha
fursa zilizopo katika taasisi zao ambazo zinawafaa vijana kuwajenga kiuchumi,baadhi
yao walikuwa ni Shirika la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO),Shirikisho la maenyesho ya kilimo(TASO),HAKIKA BANK, Taasisi yamikopo ya mashine (EFTA),VETA na mashirika yanashughulika na
vijana kama DSW, VISION FOR YOUTH (V4Y) na Shirika la kilimo cha mbogamboga,matunda na maua(TAHA).
Akielezea zaidi afisa maendeleo ya vijana,Japhet Kurwa alisema
serikali bado inaendelea kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sera ya vijana
kupitia midahalo kama hivyo ili vijana waweze kufahamu fursa zilizopo serikalini
na waweze kuzichangamkia.
Hata hivyo aliwataka vijana wao wenyewe wajitaidi
kutafuta taarifa sahihi katika ofisi mbalimbali za serikali na hasa ofisi yake
iko wazi kwaajili yao hivyo wasijisikie kama wamesahaulika katika jamii bali
wao hawatakiwi kulala ila nikukamata kila fursa wanayoiyona mbele yao.
| Afisa Maendeleo yaVijana wa Mkoa wa Arusha,Japhet Kurwa akiwakaribisha wajumbe wa mdahalo wa vijana katika ukumbi wa chuo cha ufundi Arusha (ATC). |
| Baadhi ya watoa mada wakiwa pamoja na mgeni rasmi wa mdahalo wa vijana,Jijini Arusha. |
| Baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na shughuli za vijana na vijana mbalimbali waliohudhulia mdahalo wa vijana. |
| Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mdahalo wa vijana uliofanyika Jijini Arusha. |
Friday, February 10, 2017
KANDA YA KASKAZINI YAWEKA MALENGO BORA YAKUZUIA VIFO VYA MAMA NAMTOTO
Taasisi ya White Ribbon Allince iliandaa mafunzo hayo kwa kanda ya Kaskazini kwa kushirikisha wataalamu wa afya kutoka mikoa mitatu ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara.
Ambapo wataalamu wote kutoka mikao mitatu waliweza kuwasilisha hali halisi ya vifo vya mama na mtoto kwa mikoa yao mitatu.
Aidha baada ya taarifa hizo mjadala ulifuata wakuweka malengo na mikakati zaidi itakayoenda kutekelezwa katika mikoa yote mitatu.
Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na mikoa yote mitatu ni ;kuongeza idada ya maafisa maendeleo ya jamii katika ngazi za kata,kuboresha zaidi mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya.
Pia viongozi wa hospitali wapewe elimu ya uongozi bora iliwaweze kuwaongoza vizuri waliochini yao,kuongeza vifaa tiba na upatikanaji wa damu salama,watumishi waliopo wafanye kazi kwa bidii na kuongeza wateja wa bima ya afya(CHF/TIKA) kwa kila kata.
Akisisitiza zaidi Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara bwana Eliakimu Maswi amewataka watumishi wote wa afya wabadili mitazamo yao juu yakutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuwepo na motisha kwa watumishi wa chini ili kuwapa moyo wakufanya kazi.
Taasisi hii imekuwa ikishirikiana kwa karibu na serikali katika tafiti zake wanazofanya kwa upande wa afya nakushirikisha mawazo yao katika vikao vyao wanavyofanya kwa kila kanda kwa lengo lakuboresha hali ya huduma ya fya katika jamii.
Ambapo wataalamu wote kutoka mikao mitatu waliweza kuwasilisha hali halisi ya vifo vya mama na mtoto kwa mikoa yao mitatu.
Aidha baada ya taarifa hizo mjadala ulifuata wakuweka malengo na mikakati zaidi itakayoenda kutekelezwa katika mikoa yote mitatu.
Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na mikoa yote mitatu ni ;kuongeza idada ya maafisa maendeleo ya jamii katika ngazi za kata,kuboresha zaidi mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya.
Pia viongozi wa hospitali wapewe elimu ya uongozi bora iliwaweze kuwaongoza vizuri waliochini yao,kuongeza vifaa tiba na upatikanaji wa damu salama,watumishi waliopo wafanye kazi kwa bidii na kuongeza wateja wa bima ya afya(CHF/TIKA) kwa kila kata.
Akisisitiza zaidi Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara bwana Eliakimu Maswi amewataka watumishi wote wa afya wabadili mitazamo yao juu yakutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuwepo na motisha kwa watumishi wa chini ili kuwapa moyo wakufanya kazi.
Taasisi hii imekuwa ikishirikiana kwa karibu na serikali katika tafiti zake wanazofanya kwa upande wa afya nakushirikisha mawazo yao katika vikao vyao wanavyofanya kwa kila kanda kwa lengo lakuboresha hali ya huduma ya fya katika jamii.
| Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha afya chakujadili jinsi yakupunguza vifo vya mama na mtoto, Jijini Arusha. |
| Makatibu Tawala wa mikoa mitatu ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara walishiriki pia kikao cha afya chakupinga vifo vya mama na mtoto kwa kanda ya Kaskanzini. |
| Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Eliakimu Maswi akifunga kikao cha afya kilichojadili jinsi yakuzuia vifo vya mama na mtoto kwa kanda ya Kanskazini. |
Wednesday, January 25, 2017
ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA UNEP MKOANI ARUSHA
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira bwana Erik Solheim alipowasili mkoani Arusha kwa ziara ya siku moja. |
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa kwenye picha ya pamoja na ugeni kutoka UNEP uliotembelea katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Erik Solheim akiangalia moja ya chanzo cha maji cha Olgilai wilayani Arumeru. |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Erik Solheim akizungumza na wadau wa utalii wa Mkoani Arusha juu ya masuala ya utalii na biashara haramu ya wanyapori. |
Friday, January 20, 2017
GAMBO AFANYA KIKOA NA WAFANYABIASHARA WADOGO WA MADINI
![]() |
| Wafanyabiashara wadogo wa madini wa Jijini Arusha wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,Arusha. |














