RC Akiapishwa
Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.
Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.
JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja
Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha
Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Picha ya Pamoja
Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Thursday, December 21, 2017
Wednesday, December 20, 2017
Shule binafsi za Sekondari zatakiwa kufuata sheria ya elimu.
Katibu Tawala Msaidizi upande wa elimu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya usimamizi wa sheria ya elimu kwa shule binafsi. |
Shule zote binafsi za mkoa wa Arusha zimetakiwa kufuata
sheria ya elimu ya mwaka 2012 ya usimamizi wa upandaji wa
madarasa kwa wanafunzi wa shule hasa za Sekondari.
Akitoa rai hiyo katibu tawala masaidizi upande wa elimu
bwana Gift Kyando, amesema serikali
imeweka utaratibu wa upimaji wa wanafunzi kwa darasa la nne, darasa la
saba,kidato cha pili na kidato cha nne.
“Hakuna utaratibu wakumpima mwanafunzi wa kidato cha
tatu kwenda kidato cha nne kama inavyofanywa na baadhi ya shule binafsi kwa
kuweka wastani wa alama za masomo kwa wanafunzi na ambae hata fikisha kiwango
hicho hufukuzwa shule au kuamliwa kurudia kidato”.
Amesema serikali haitafumbia macho kwa shule yoyote
itakayokiuka sheria hiyo ya elimu nakuwataka wakuu wote wa shule wanaoendesha
shule zao kwa kukiuka utaratibu huo kuacha mara moja na pia amewasihi wazazi
wote waendelee na maandalizi ya watoto wao wanaoingia kidato cha nne bila hofu
yoyote.
Pia amesema serikali itaendelea kuzifuatilia shule zote
za binafsi hasa zilizobainika kukiuka sheria hiyo ili kuhakikisha wanafunzi
hawafukuzwi au kurudia madarasa bila utaratibu uliowekwa na serikali.
Amewataka wazazi wote ambao watoto wao watakataliwa
kuendelea na masomo kwa kigezo cha kikosa wastani wa alama za shule husika,
watoe taarifa haraka katika ofisi za elimu za mkoa wa Arusha
kwa hatua zaidi.
Friday, August 11, 2017
Katibu Mkuu TAMISEMI Eng.Musa Iyombe ateta na watumishi wa umma wa mkoa wa Arusha.
Katibu Mkuu TAMISEMI,Eng.Musa Iyombe,akizungumza na katibu tawala mkoa Richard Kwitega(kushoto) na katibu tawala wilaya ya Arusha David Mwakiposi(kulia) baada ya kikao na watumishi wa mkoa wa Arusha. |
Baadhi ya watumishi wa umma wa mkoa wa Arusha,waliohudhuria kikao cha Katibu Mkuu TAMISEMI,Eng. Musa Iyombe(hayupo pichani) katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa,jijini Arusha. |
Friday, July 28, 2017
TIMU YA RIADHA YA TAIFA YAAGWA RASMI MKOANI ARUSHA
Katinu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya riadha ya taifa, jijini Arusha. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,akikabidhi fedha kwa kocha wa timu ya riadha ya Taifa alipokuwa akiiaga rasmi kwa ajiri ya safari ya London. |
Timu ya riadha ya taifa imekabidhiwa kiasi cha shiling
laki tano kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa
wa Arusha kama mchango wakuiunga mkono timu hiyo na kuitakia kila la kheri
katika mashindano ya dunia.
Akitoa zawadi hiyo katibu tawala wa mkoa wa Arusha
Richard Kwitega amesema, mkoa umeguswa sana na juhudi zinazooneshwa na timu
hiyo katika mashindano mbalimbali hivyo kupitia ofisi yake imetoa kiasi hicho
ili kuwaunga mkono wanariadha hao.
“Ofisi ya mkoa imeona haitakuwa sahihi sana kuiacha timu
hii iondoke hivi hivi bila yakuitakia kheri ya mafanikio katika mashindano hayo
ya riadha ambayo niya dunia, wakati imeweka kambi mda wote katika mkoa huu”.
Amewahasa kuwa wanapotoka hapo wawe na mawazo ya ushindi
tu na wakazingatie yale yote waliyofundishwa wakati wakiwa kambini na walimu
wao.
Aidha, amewataka wanaobaki kambini waendelea na mazoezi
kwa juhudi zaidi na wasife moyo kwani mashindano yoyote yanaitaji juhudi na
nidhamu ya hali ya juu.
Akitoa salamu za shukrani mmoja wa washiriki wa timu ya
taifa Alex Siumbu amesema anaamini wanaenda kushinda na si vinginevyo kwani
wameweza kufanya mazoezi kwa mda mrefu na watanzingatia maelekezo yote waliyopewa
na walimu wao.
Timu hiyo ya riadha yenye washiriki 8 inatarajiwa
kuondoka jijini Arusha Julai 29 kuelekea Dar es Salaama kwa maandalizi yakuangwa
kitaifa Julai 31 na kuanza safari yakuelekea London Uwingereza Agosti 1 kwenye
mashindano ya dunia.
Baadhi ya wanariadha wa timu ya taifa ya riadha wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha( hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha za kuwaaga rasmi. |
Friday, July 14, 2017
MAANDALIZI YA NANE NANE JIJINI ARUSHA YAMEPAMBA MOTO.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera,akifunga kikao cha maandalizi ya sherehe za nane nane, katika viwanja vya maonyesho hayo,jijini Arusha. |
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera amesema maonyesha
ya kilimo na mifugo, maarufu kama nane nane mwaka huu kwa kanda ya Kaskazini
yataongoza kwa ubora kwa nchi nzima.
Aliyasema hayo alipokuwa akifunga kikao cha maandalizi ya
sherehe hizo za nane nane kwa kanda ya Kaskazini ambayo yanajumuisha mikoa
mitatu ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro.
Amesema kwa Serikali hii ya awamu ya tano niwajibu
wakila mtu kufanya kazi kwa bidii nakuacha kufanyakazi kwa mazoea, ili kila
mipango iliyowekwa katika maandalizi hayo yafanikiwe na kanda hii kushika
nafasi ya kwanza nakua mfano kwa nchi nzima.
Akisisitiza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
ameziagiza TANESCO na AUWSA kuhakikisha maji na umeme vinapatikana katika
maeneo husika ya viwanja vya maonyesho ya nane nane ndani ya wiki moja.
Pia, Gambo amemwagiza mkuu wa wilaya ya Arusha kuunda tume yakufuatilia taratibu za matumizi
ya viwanja hivyo hasa katika wakati ambao sio wa maonyesho, ili kusaidia kupata
taarifa kamili itakayosaidia kutoa hali halisi kabla ya makabidhiano baina ya
taasisi iliyokuwa ikisimamia maonyesho hayo TASO na ofisi ya mkuu wa mkoa wa
Arusha.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Gelasius Byakanwa
amesema pia katika kikao kijacho nivizuri taarifa ya mapato na matumizi kwa
mwaka jana na mwaka huu isomwe kwa wajumbe ili waweze kupata hali halisi ya
mapato hayo.
Maonyesho ya nane mwaka huu yataratibiwa na ofisi za
makatibu tawala wa mikoa yote mitatu ya kanda ya Kaskazini kwa ushirikiano na Wizara
ya Kilimo, Mifugo na Uvivu na mpaka sasa ni makampuni 33 tu ndio yamedhibitisha ishiriki katika
maonyesho hayo, wananchi wote bado wanahamasishwa kushiriki kuanzia siku ya
mwanzo hadi mwisho.
Wakuu wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wakikagua maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha. |
Baadhi ya viongozi wa kutoka mikoa ya kanda ya Kaskazini waliohudhuria kikao cha maandalizi ya maonyesho ya nane nane,jijini Arusha. |
Wednesday, July 12, 2017
KATIBU TAWALA,RICHARD KWITEGA ATEMBELEA KITUO CHA SOS CHILDREN VILLAGE
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega, akiwa pamoja na baadhi ya vijana wanaolelewa katika kituo cha SOS Children Village tokea wakiwa na umri wa miaka 3 na baadhi ya walezi wao,Ngaramtoni. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega amesema
serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wa karibu sana na taasisi ya SOS Children Village kwenye
shughuli wanazofanya hususani zakusaidia watoto wasio na wazazi.
Aliyasema hayo alipotembelea kituo hicho kwa lengo
lakutaka kufahamu zaidi namna taasisi hiyo inavyofanya kazi ilikuona nikwajinsi
gani serikali inaweza kushirikiana nayo katika kuwalea watoto hao kwakuwa na
wao niwatanzania wanahaki zote zakuhudumiwa na serikali yao.
“Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi hii
katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma iliyo bora kwa watoto wetu
hawa na wao waweze kujisikia kweli serikali yao ipo pamoja nao.”
Aidha, amepongeza taasisi hiyo kwa kutoa malezi mazuri
kwa watoto hao hasa kwakuwalea kama wapo na wazazi wao halisi hasa kwakuwapa
elimu na huduma ya afya.
Bwana Kwitega amesisitiza zaidi kuwa serikali kwa kuanza
inaweza kutoa ushirikiano kwa kuleta wataalamu wa elimu yani walimu na
wataalamu wa afya ambao watakuwa waajiriwa wa serikali lakini wakitoa huduma katika
kituo hicho.
Akitoa historia fupi ya taasisi hiyo,Mkurugenzi wa
taasisi hiyo bwana Francis Msollo alisema kituo hicho kilianza mwaka 2000
kikiwa na nyumba 10 tu zakuishi watoto hao lakini mpaka sasa wamefikisha nyumba
15 na watoto 200.
Pia alisema mbali yakuwalewa watoto hao wasio na wazazi,
taasisi inatoa pia msaada kwa wale watoto wenye mzazi mmoja kwakuwapa ufadhiri
wa elimu inayotolewa katika taasisi hiyo.
Taasisi hiyo pia imetoa nafasi kwa watoto wanaozunguka
maeneo ya taasisi hiyo kupata elimu inayotolewa katika kituo hicho.
Akisisitiza zaidi bwana Msollo alisema, Changamoto wanayokabilina
nayo kwasasa nikwabaadhi ya wafadhili kujitoa katika kutoa fedha zakutoa huduma
za afya na elimu na hivyo kuiomba serikali iangalie naoma yakusaidia taasisi
hiyo ili watoto hao waendelee kupata elimu bora na afya.
Msollo amesema, mipango ya baadae ya taasisi hiyo
nikuboresha mabweni ya watoto hao iliwaweze kuchukua watoto wengi zaidi
wakiwemo watoto wa mbali na mazingira hayo, pia usafiri kwa watoto hao
wanaotoka mbali huku elimu itolewe zaidi katika jamii juu yakuwahudumia watoto
hao yatima katika maeneo yao.
Taasisi ya SOS Children Village iliaanzishwa mwaka 1984
huko Zanzibar na baadae kufungua vituo vingine vinne katika mikoa ya Mwanza,Dar
es Salaam, Arusha na Iringa, hadi sasa imeshaeenea katika nchi mbalimbali kama
South Afrika na Uganda.
Katibu Tawala Richard Kwitega, akimsikiliza mmoja wa vijana aliyelelewa na kituo cha SOS Children Village Bi. Anna Lomayani na sasa anafamilia yake. |
Bwana Kwitega, akiwasalimia baadhi ya watoto wa shule ya awali wa kituo cha SOS Children Village. |
Thursday, July 6, 2017
MAONYESHO YA NANE NANE 2017.
Katibu Tawala akitoa maelezo juu ya maadhimisho ya siku ya nane nane kwa kanda ya Kaskazini. |
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega amesema kuwa maonyesho ya wakulima
maarufu kama nane nane ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja wa Themi
Njiro yataendelea kuwepo kama kawaida.
Ameyasema hayo baada yakutokea sitofahamu kwa wananchi kutokana
na iliyokuwa taasisi yakusimamia maonyesho hayo (TASO) kuzuiliwa kuendelea
kuratibu maonyesho hayo.
Aidha, amesema kwa mwaka huu maonyesho hayo yataratibiwa
kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Sekretarieti za Mikoa
ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara pamoja na TASO.
Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ikiwa ndio mwenyeji
wa maonyesho hayo ndio imepewa jukumu lakusimamia uwandaaji wa shughuli zote
katika viwanja hivyo.
Ametoa wito kwa washiriki wote wa maonyesho hayo kwa
mwaka huu 2017 kuanza maandalizi mapema
ikiwemo ulipaji wa ada ya ushiriki katika ofisi zilizokuwa za TASO ndani ya
viwanja vya nane nane ambapo kwa sasa kuna maafisa walioteuliwa kutoka katika
Wizara na Sekretarieti ya Mkoa kutumia ofisi hizo kwa shughuli hizo.
Pia shughuli nyingine za Maandalizi zikiwemo kuwasilisha
mahitaji ya idadi ya waoneshaji, Magari, na taarifa nyingine zifanyike katika
ofisi za TASO kabla ya Julai 20,2017.
Kwa mwaka huu maonyesho hayo yatabeba kauli mbiu isemayo
“Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi
wa kati”,ambayo yataanza rasmi Agosti moja,2017 nakumalizika Agosti 10,2017.