RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Saturday, March 24, 2018

Zaidi ya Wamama 600 Wakopeshwa Mitaji ya Bila Riba

Muheshimiwa Jenista Muhagama,Muheshimiwa Antony Mavunde na Muheshimiwa Mrisho Gambo wakikabidhi mfano wa Hundi ya Milioni 120 kwa akinamama 600,Jijini Arusha.

Wanawake wa Arusha watakiwa kutumia vizuri mikopo yao kwa kuwekeza kwenye shughuli  mbalimbali za maendeleo na zitakazo zalisha kwa wingi na kuwaletea mapato yakutosha katika familia zao.

Ameyasema hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Jenista Muhagama alipokuwa akikabizi hundi ya milioni 120 ya mkopo wa akinamama wajasiliamali, Jiji la Arusha.

Amewataka wanawake waonyeshe kuwa wanaweza kuinuka kiuchumi na kuacha utegemezi huku wakitekeleza majukumu yao katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla.

“Mikopo hiyo mnayoenda kupewa ichukulieni kama mmepata tunda la embe katika mti wa miba,yani haitakaa itokee tena mkapatiwa mikopo hiyo kwa mara nyingine”.alisema

Aidha,amewahasa wakatumie vizuri  mikopo hiyo na waache kwenda kununua vitu ambavyo havitawasaidia katika kujiletea maendelea yao na familia zao.

Serikali ya awamu ya tano imelenga katika kuhakikisha matunda ya nchi yanaliwa na kila mtanzania,hivyo fursa hiyo ya wanawake kupatiwa mitaji kwa mikopo isiyo na riba nimkakati mzuri wakutelekeza ilani ya chama cha mapinduzi.

Amesema wizara yake ipo tayari kuwasaidia wakimama wote watakao fanikiwa kumaliza marejesho yao na atawasaidia kupata mikopo mingine ya riba nafuu huku wakiwa katika vikundi.

Pamoja na akimama kipatiwa hiyo mikopo wanaweza pia kutafuta fursa kubwa zaidi katika miradi mikubwa inayofanywa na serikali,ili na wao waweze kukua katika biashara zao.

Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa juhudi alizozifanya za kusaida makundi maalumu ya vijana,wanawake na wenye ulemevu katika kuwatengenezea ajira zaidi ya 200.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema akinamama ni kundi kubwa sana linalotegemewa kwa asilimia kubwa katika ngazi za familia na jamii kwa ujumla,hivyo aliona hana budi kutafuta namna yakuwawezesha ili waweze kujikwamua katika maisha yao.

Amewataka wenye mapenzi mema waendelee kusaidia akinamama katika Nyanja ya kujikwamua kiuchumi ile pale wanapokosa usaidizi basi waweze kusimama wao kama wao na kuendesha maisha yao na wategemezi wao.

Akisisitiza zaidi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,amesema mwanamke nisawa na hewa ya oxjeni pale inapokosekana inaleta maafa makubwa na pengine kupoteza kabisa uhai wa binadamu.

Akitoa salamu za pongezi  Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators (TATO) bwana Wilbad Chambulo kama mmoja wa wadau amesema alichofanya Gambo ni jambo la kuigwa na watu wengine na yeye atachangia kiasi cha milioni 20 ili wakimama wengine 100 waweze kukopeshwa.

Mikopo isiyokuwa na riba ya kuwezesha makundi mbalimbali katika Mkoa wa Arusha ilianza kwa vijana 200 kukopeshwa pikipiki na baada ya kufanya marejesho yao kiasi cha milioni 120 kimetolewa kuwakopesha akinamama 600 kama mtaji wakufanya  biashara mbalimbali.

Baadhi ya Wadau na akinamama walioudhuria sherehe za kuwakabidhi mikopo akinamama 600 wa Jiji la Arusha.


Friday, March 23, 2018

Madini ya Vito Kuongezewa Thamani

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akisikiliza maelezo ya namna yakung'arisha madini kutoka kwa Mkufunzi Bi.Mariam Swalehe wa kituo cha kuongeza thamani Madini aina ya Vito,Jijini Arusha.


Kituo cha kuongeza thamani ya madini (Tanzania Geological Centre),kimejipanga kutoa mafunza kwa wingi kwa wajasiliamali  ya namna yakuongeza thamani ya madini ya Vito.
Akitoa pongezi kwa kituo hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema niwakati sasa kwa watanzania kujivunia na kunufaika na madini yao.
Amesema kituo hicho kimefanya vizuri sana kuanzisha mafuzo hayo kwa wajasiliamali ili kuwaongezea ujuzi wa utambuzi  wa madini ya vito na hii itasaidia kupunguza udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watu.
“Mafunzo haya mnayotoa yatasaidia kupunguza udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wa  madini kwa kutengeneza madini feki nakuwauzia wateja wao.”alisema
Amemshauri mratibu wa kituo cha kuongeza thamani kuanza kufikiria namna ya kuwa na chapa za Tanzania katika madini ili kujitangaza zaidi ndani na nje ya nchi kuliko kutokuwa nayo hii inapelekea nchi nyingine kupata jina katika soko kwa kutumia madini yetu.
Aidha,amesema ameshafanya mawasiliano na balozi wa India kuwaomba kuwafadhiri baadhi ya wataalamu kwenda India kupata mafunzo zaidi ya namna yakutambua na kuyaongezea thamani madini na balozi amesharidhia.
Gambo ameshauri pia wadau wa madini nao wangeshirikishwa juu yakudhamini baadhi ya wajasiliamali kupata elimu hiyo na hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wajasiliamali watakaopa elimu hiyo.
Pia,Mratibu wa kituo hicho bwana Erick Mpesa amesema,kituo hicho kilianzishwa 2014 na mpaka sasa tayari wanafunzi 300 wameshahitimu mafunzo hayo.
Amesema bado wanaendelea na juhudi za kuandaa makumbusho itakayotumika kutunza madini yote yanayopatikana hapa nchini,hii itasaidia hata kama madini yetu yataisha lakini kumbukumbu inatakiwa kuwepo kwa vizazi vijavyo.
Mkuu wa mkoa yupo katika ziara ya kutembelea viwanda vya Arusha kwa siku 3 na lengo ni kusikiliza changamoto zinazowakabiri wawekezaji kwa kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano nikuhakikisha nchi inaingia katika hatua ya viwanda.




Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo akimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Kuongeza Thamani Madini Bwana Erick Mpesa akimwelezea juu ya utambuzi wa madini unavyofanywa na kituo hicho, pembeni yake ni Mkurugenzi wa madini Bwana Adamu,Jijini Arusha.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akimsikiliza Mkufunzi Peter John akimwelezea namna wanavyochonga bidhaa kwa kutumia mawe,Jijini Arusha.


Katibu Tawala Mkoa Richard Kwitega,akikagua moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda cha Sunkist,Jijini Arusha.


Monday, March 12, 2018

Wajasiliamali wa Vinyago Kukuza Soko

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe,akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akimwelezea namna soko la vinyago linavyofanya kazi, pembeni ni Mwenyekiti wa soko hilo Elias Rajabu.

Waziri wa habari, utamaduni,sanaa na michezo Dokta Harrison Mwakyembe amewataka wajasiliamali wa vinyago kutafuta zaidi soko la bidhaa zao za asili ili kukuza kipato na kuendelea kutangaza utalii wa utamaduni.

Ameyasema hayo alipokuwa akuzunguza na wajasilimali wautalii wa utamaduni katika soko la Masai,jiji Arusha.Amesema bidhaa za utalii wa utamaduni ni nembo tosha yakutangaza nchi yetu.

“Ni kweli kuna Changamoto katika ujasiliamali huu wa utalii wa utamaduni hususani kwenye tozo mbalimbali mnazotozwa na mamlaka husua.”

Serikali ipo tayari kwenye mchakato wakutatua Changamoto hii ya tozo na kuona ni namna gani soko la vinyago nchini Tanzania linakuwa na kujulikana zaidi kimataifa, kuliko kwa sasa soko kuu linajulikana lipo jijini Nairobi wakati wazalishaji wakubwa ni  watanzania.

Dokta Mwakyembe alikuwa kwenye ziara ya siku 3 Mkoani Arusha,ambapo ameweza kufungua redio mpya ya kijamii (TBC FM),aliweza kutembelea kituo cha redio cha Sunrise,alifungua mkutano wa maafisa habari na mawasilino serikali,ameweza kukutana na wadau wa utamaduni,sanaa na michezo na ameweza kutembelea soko la vinyago la jijini Arusha.

Waziri Mwakyembe akizungumza na baadhi ya watalii waliofika katika soko la vinyago,jijini Arusha.


Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe akitazama moja ya bidhaa zinazopatikana katika soko la vinyago jijini Arusha.


Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe, akipokea zawadi ya kikombe kilichotengenezwa kwa shanga kwa mmoja wa wajasiliamali wa soko la vinyago jijini Arusha.


Tuesday, March 6, 2018

Bodaboda 107 Wamikili Pikipiki

Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Mwigulu Nchemba,akimkabidhi bwana Peter Urio kadi ya Pikipiki,Mkoani Arusha.

Waendesha bodaboda mkoani Arusha wapewa miezi mitatu kuhakikisha wanajifunza sheria na taratibu za barabara bila kusumbuliwa na polisi wa barabarani.

Akitoa kauli hiyo,Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Mwigulu Nchemba katika kikao chake na waendesha bodaboda wa mkoa wa Arusha alipokuwa akiwagawia kadi za umili wa bodaboda  kwa madereva 107 waliofanikiwa kumaliza mkopo wa mradi wakukopesha pikipiki ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kauli hiyo imetolewa na mheshimiwa waziri baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoa ombi maalum kwake lakuwaruhusu madereva bodaboda hao kujifunza sheria kwanza kisha ndio polisi waanze utaratibu wakuwakamata wale wote watakaokuwa wamekiuka sheria za barabarani.

Mwigulu Nchemba amewasihi bodaboda wote nchini kuchukulia hii kazi kama yenye heshima ili iweze kuwabadilisha maisha yao na tegemeze wao.

Aidha,amesisitiza utoaji wa leseni kwa bodaboda utazingatia kwa wale ambao watakuwa wanamiliki kofia mbele na hata akiwa na cheti pia atapatiwa leseni,pia abiria atakaekaidi kuvaa kofia basi atapatiwa adhabu yeye nasio dereva kama ilivyokuwa awali.

Akichangia zaidi juu ya mradi huu,Mwiguli Nchemba atachangia kiasi cha shilingi milioni 10 ilikusaidia vijana wengine waweze kukopeshwa pikipiki kwa wingi.

Pia, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewaambia bodaboda kuwa wanaweza kutumika katika kubeba watalii ikiwa tu wataweza kufuata sheria na taratibu za barabarani.

Amewapongeza watendaji kata na maafisa tarafa wa Jiji la Arusha kwakuonyesha ushirkiano mkubwa katika kufanikisha makusanyo na kwa wakati, na kiasi cha shilingi milioni 306 tayari zimesharudishwa na milioni 200 zitatumika kukopesha wamama wajasiriamali wadogo kwa mkopo wa shilingi laki 2 kwa wamama 500.

Amesema kiasi cha pesa kinachobaki cha zaidi ya milioni 100 kitatumika kukopesha waendesha bodaboda wengine,hii itasaidia kuwawezesha vijana wengi kumuliki pikipiki zao wenyewe badala yakutegemea pikipiki za watu wengine ambazo zinawabana sana.

Kamanda wa polisi kitengo cha barabarani Joseph Buberwa,amewataka bodaboda kuhakikisha wanatii sheria bila shuruti,wapunguze spidi barabarani hususani kwenye makazi ya watu.

Amesema kuwa polisi barabarani hawatawakamata bodaboda ambao hawana leseni lakini wana cheti cha udereva na watawapa mda wakuhakikisha wanapata lesenina amewapongeza madereva 250 waliofanikiwa kuhitimu mafunzo ya udereva.

Akisisitiza zaidi mwenyekiti waumoja wa madereva bodaboda (UBOJA) bwana Mauridi Makongoro,amesema mradi huo umewanufaisha sana bodaboda wengi kwani umewatoa katika mazingira yakuendesha bodaboda za watu wengine na sasa wanamiliki zao wenyewe na wameweza kuingiza kipato chakutosha.

Mradi huu ulianzishwa mwaka 2017 na mheshimiwa Gambo kwa lengo lakuwakwamua bodaboda wa Jiji la Arusha katika changamoto yakukosa mtaji wakumiliki pikipiki zao, vijana 200 walifanikiwa kukopeshwa pikipiki hizo na kati yao 107 wamemaliza mkopo nakukabidhiwakadi za umiliki wa pikipiki na wengine wanaendelea na marejesho.


Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba,akiwa kwenye picha ya pamoja,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,viongozi wa CCM Wilaya ya Arusha na bodaboda wa Jiji la Arusha.


Baadhi ya waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha wakimsikiliza Mwigulu Nchemba(hayupo pichani) kwenye kikao chakukabidhi kadi za umiliki wa bodaboda,Jijini Arusha.


Friday, March 2, 2018

Watoto Wenye Mahitaji Maalum Washinda Medali





Hawa ni wawakilishi wa mashindano ya Olimpiki Maalum Kimataifa, Kulia ni Simon Oloije,katika ni Rehema Soingei na Elizabeth Kisaka,kutoka Arusha.

Watoto wenye mahitaji maalumu(ulemavu wa akili) 34 watunukiwa medari 32 baada yakuibika washindi katika mashindano  ya Olimpiki MaalumuTanzania ali maalufu kama (SOT) yaliyofanyika mapema Zanzibar.

Akiwatunuku medari hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha,Emmanuel Maundo amesema nijambo lakujivunia sana kwa mkoa wetu kuibuka washindi katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na riadha,na kuweza kupata wawakilishi katika mashindano ya kimataifa.

“Ninafuraha sana kuona watoto wetu wenye ulemavu wa akili wameweza kuuwakilisha vizuri mkoa wetu katika mashindano haya, na wameweza kuonyesha kuwa hata wao wanaweza kufanya vizuri sana katika michezo mbalimbali.”alisema

Emmanuel Maundo(Mwakilishi wa Katibu Tawala Arusha-mwenye nguo Nyeupe)akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu wa akili,wadau,walimu na wazazi,mbele ya ofisi ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha.

 Amewasihi sana wazazi ambao bado wanaendela kuwaficha watoto kama hao waache mara moja kwani hata wao bado wana fursa kubwa katika jamii yetu,hivyo wanatakiwa kupewa nafasi kama ilivyo kwa watoto wengine.

Aidha, amezitaka halmashauri zote za mkoa wa Arusha kuhakikisha zinatenga bajeti maalumu yakuendesha michezo kwa watoto wenye ulemavu kama ilivyo kwa watoto wengine na kuhakikisha zinashiriki katika mashindao yajayo.


Serikali inatambua vizuri sana mahitaji ya kundi hili la watoto wenye mahitaji maalumu ndio maana ikatenga bajeti yakutosha mashuleni ili waweze kupata chakula chakutosha asubuhi na mchana.

Emmanuel  Maundo akikabidhi cheti cha chukrani kwa bwana,Yuzra Mushree kutoka Kampuni ya A and B Limited,waliotoa mchango wao mkubwa katika kufanikisha safari ya timu ya walemavu wa Akili.

Akiongezea zaidi,amesema ofisi ya mkuu wa Mkoa Arusha itaendelea kuwa bega kwa bega na timu hiyo nakutoa ushirikiano kila mara ili kuwasaidia watoto hao waweze kuendelea na michezo yao.


Pia mratibu wa SOT Bwana Antony Mushi, amesema timu ya watoto hao walemavu wa akili imeweza kuibuka na medari 6 za Dhahabu,12 za Fedha na 14 za Shaba nakufanikiwa kutoa watoto watatu ambao watashiriki mashindano yakimataifa yatakayofanyika Machi 2019,huko Abu Dhabi Uarabuni.

Amewashukuru wafadhili mbalimbali waliojitokeza katika kusaidia mahitaji mbalimbali ya timu hiyo hususani tiketi za mabasi kwenda Zanzabar na kurudi,vyakula na vifaa vya michezo.Amehimiza wasichoke kusaidia kwani bado uhitaji nimkubwa na kuomba na wafadhili wengine wajitokeze zaidi.

Afisa Michezo wa Mkoa Mwamvita Onoka, nae amesema kama mkoa atahakikisha mashindao hayo ya watoto wenye ulemevu wa akili yanafanyika kila mwaka kwa Mkoa wa Arusha.

Afisa Michezo Mkoa wa Arusha Mwamvuta Onoka akimvisha medali mmoja wa watoto wenye ulemeavu wa akili walioshiriki mashinda ya michezo mbalimbali,Zanzibar.


Amesema michezo kwa watoto hao nimuhimu sana kwa afya zao hivyo hamna budi kuyafanya kila mwaka badala yakusubiri kila baada ya miaka 3 au 4.


Olimpiki maalumu kwa Mkoa wa Arusha ilianza mwaka 1990 kwa mashindano hayo kufanyika hapa hapa Arusha na baadae yaliendelea katika mikoa mingine nchini.

Emmanuel Maundo akimvisha medali mmoja wa watoto walioshiriki mashindano ya Olimpiki Maalumu,Zanzibar.