RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Saturday, February 18, 2017

VIJANA JIJINI ARUSHA WAPEWA SIRI YA MAFANIKIO YAO.

Mkuu wa wilayaya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro akizungumza na baadhi ya vijana wa jiji la Arusha wakati akifungua mdahalo wa vijana kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro amefungua mdahalo wa vijana wa jijini Arusha kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha(ATC),mdahalo ulikuwa na lengo lakutoa elimu kwa vijana juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Arusha.


Daqarro aliwahamasisha vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vilivyosajiriwa ili waweze kupata mikopo ya serikali itakayowasaida katika shughuli mbalimbali zakuinua uchumi wao badala ya wao kukaa vijiweni nakulalamika hakuna ajira.

“Ni vema vijana mkajiunga kwenye vikundi vya watu 8 hadi 30 na mkavisajiri ili muweze kupata mikopo kutoka serikalini kuliko kukaa vijiweni nakusubiri ajila ziwafuate au kulalamika hakuna ajira”.

lisisitiza kuwa vijana pia watafute fursa kwenye soko la jumuiya ya afrika masharika kwani wakilala wao ndio watageuzwa kuwa soko kwasababu fursa zote zitachukuliwa na wageni.

Pia amewahasa wasipendi urahisi wamaisha kwakutaka mafanikio haraka kwa njia zisizo halali kwani ndio zinawapelekea wajiingize katika biashara harama kama zakuuza na kutumia madawa ya kulevya.

Hata hivyo taasisi mbalimbali nazo ziliweza kuonyesha fursa zilizopo katika taasisi zao ambazo zinawafaa vijana kuwajenga kiuchumi,baadhi yao walikuwa ni Shirika  la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO),Shirikisho la maenyesho ya kilimo(TASO),HAKIKA BANK, Taasisi  yamikopo ya mashine (EFTA),VETA na mashirika yanashughulika na vijana kama DSW, VISION FOR YOUTH (V4Y) na Shirika la kilimo cha mbogamboga,matunda na maua(TAHA).

Akielezea zaidi afisa  maendeleo ya vijana,Japhet Kurwa alisema serikali bado inaendelea kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sera ya vijana kupitia midahalo kama hivyo ili vijana waweze kufahamu fursa zilizopo serikalini na waweze kuzichangamkia.

Hata hivyo aliwataka vijana wao wenyewe wajitaidi kutafuta taarifa sahihi katika ofisi mbalimbali za serikali na hasa ofisi yake iko wazi kwaajili yao hivyo wasijisikie kama wamesahaulika katika jamii bali wao hawatakiwi kulala ila nikukamata kila fursa wanayoiyona mbele yao.

Afisa Maendeleo yaVijana wa Mkoa wa Arusha,Japhet Kurwa akiwakaribisha wajumbe wa mdahalo wa vijana katika ukumbi wa chuo cha ufundi Arusha (ATC).

Baadhi ya watoa mada wakiwa pamoja na mgeni rasmi wa mdahalo wa vijana,Jijini Arusha.

Baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na shughuli za vijana na vijana mbalimbali waliohudhulia mdahalo wa vijana.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mdahalo wa vijana uliofanyika Jijini Arusha.

Friday, February 10, 2017

UZINDUZI RASMI WA SIKU YA MAZOEZI MKOANI ARUSHA



KANDA YA KASKAZINI YAWEKA MALENGO BORA YAKUZUIA VIFO VYA MAMA NAMTOTO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akifungua kikao cha afya  kwa kanda ya Kaskanzini chakujadili jinsi yakupunguza vifo vya mama na mtoto kilichoandaliwa na taasisi ya White Ribbon Allince,Jijini Arusha.
Taasisi ya White Ribbon Allince iliandaa mafunzo hayo kwa kanda ya Kaskazini kwa kushirikisha wataalamu wa afya kutoka mikoa mitatu ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara.

Ambapo wataalamu wote kutoka mikao mitatu waliweza kuwasilisha hali halisi ya vifo vya mama na mtoto kwa mikoa yao mitatu.

Aidha baada ya taarifa hizo mjadala ulifuata wakuweka malengo na mikakati zaidi itakayoenda kutekelezwa katika mikoa yote mitatu.

Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na mikoa yote mitatu ni ;kuongeza idada ya maafisa maendeleo ya jamii katika ngazi za kata,kuboresha zaidi mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya.

Pia viongozi wa hospitali wapewe elimu ya uongozi bora iliwaweze kuwaongoza vizuri waliochini yao,kuongeza vifaa tiba na upatikanaji wa damu salama,watumishi waliopo wafanye kazi kwa bidii na kuongeza wateja wa bima ya afya(CHF/TIKA) kwa kila kata.

Akisisitiza zaidi Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara bwana Eliakimu Maswi amewataka watumishi wote wa afya wabadili mitazamo yao juu yakutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuwepo na motisha kwa watumishi wa chini ili kuwapa moyo wakufanya kazi.

Taasisi hii imekuwa ikishirikiana kwa karibu na serikali katika tafiti zake wanazofanya kwa upande wa afya nakushirikisha mawazo yao katika vikao vyao wanavyofanya kwa kila kanda kwa lengo lakuboresha hali ya huduma ya fya katika jamii.


Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao cha afya chakujadili jinsi yakupunguza vifo vya mama na mtoto, Jijini Arusha.

Makatibu Tawala wa mikoa mitatu ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara walishiriki pia kikao cha afya chakupinga vifo vya mama na mtoto kwa kanda ya Kaskanzini.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Eliakimu Maswi akifunga kikao cha afya kilichojadili jinsi yakuzuia vifo vya mama na mtoto kwa kanda ya Kanskazini.

Wednesday, January 25, 2017

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA UNEP MKOANI ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira bwana Erik Solheim alipowasili mkoani Arusha kwa ziara ya siku moja.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Erik Solheim na viongozi wengine walipofanya kikao katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa kwenye picha ya pamoja na ugeni kutoka UNEP uliotembelea katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira bwana Erik Solheim akionyeshwa moja ya mahakama itakayotumika katika kusikiliza kesi mbalimbali na Mkuu wa mahakama ya Afrika kwa Arusha bwana Samuel Akorimo katika mahakama ya Afrika iliyopo Arusha

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Erik Solheim akiangalia moja ya chanzo cha maji cha Olgilai wilayani Arumeru.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Erik Solheim akizungumza na wadau wa utalii wa Mkoani Arusha juu ya masuala ya utalii na biashara haramu ya wanyapori.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Bwana Erik Solheim akiangalia baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda cha Banana Investment alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo lakuangalia mfumo wa usafishaji maji na utunzaji wa mazingira wa kiwanda hicho.

Friday, January 20, 2017

GAMBO AFANYA KIKOA NA WAFANYABIASHARA WADOGO WA MADINI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiwa kwenye kikaona wafanyabiashara wadogo wa madini wa Jijini Arusha,kulia kwake ni Kamishina wa madini kanda ya Kaskazini Adam Juma na kushoto kwake ni kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amewapiga marufuku polisi wa Mkoani Arusha kuwasumbua ovyo wafanyabiashara wadogo wa madini(Brokers) katika maeneo yao yakufanyia biashara bila kufuata utaratibu maalumu.
Ameyasema hayo alipokuwa akifunga kikao chake na wafanyabiashara hao katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kikiwa na lengo lakusikiliza kero zao na kuongeza ushirikiano baina ya wafanyabiashara hao na serikali yao ya Mkoa wa Arusha.
“Ninamwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kuanzia sasa kusimamisha zoezi hili lakuwasumbua hawa wafanyabiashara wadogo wa madini katika maeneo yao ya biashara bila kufuata taratibu”.
Aidha Gambo amewaagiza Kamishina wa Mamlaka ya mapato (TRA) Arusha na ofisi ya madini kanda ya Kansazini kuandaa mpango maalumu wakutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo wa madini wa Mkoa wa Arusha juu ya  utoaji wa leseni za madini na ulipaji wa kodi.
Alisema hayo baada ya wafanyabiashara hao kutoa malalamiko yakutoelewa taratibu za upatikanaji  wa leseni za madini na pia hawana elimu tosha juu ya ulipaji kodi kwani wengi wanaona wanatozwa kodi kubwa ambazo haziendani na hali halisi ya biashara zao wanazofanya.
Akisisitiza zaidi Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema jeshi la polisi la Mkoa wa Arusha litaendelea kudumisha ulinzi na usalama kwa wananchi wote na mali zao.
Hivyo kawataka wafanyabaishara wadogo wa madini wa Mkoa wa Arusha kuwa na imani na jeshi lao la polisi kwani litaendelea kuwalinda wao na malizao na hata kwa wale waliokamatwa nakunyang’anywa madini yao, ofisi yake itafuatilia iliwanaostaili kurudishiwa watapewa mali zao.
Kamishina wa mamlaka ya mapato Arusha(TRA) bwana,Ambili Mbaluku amesema ni vizuri wafanyabaishara hao wakajitaidi kulipa kodi kadri ya mapato yao kwasabau serikali inategemea kodi hizo katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii na wao watajitaidi kutoa elimu zaidi juu ya ulipaji kodi mzuri.
Pia kamishina wa madini kanda ya Kansazini Adam Juma amesema nivizuri wafanyabaishara hao wakakata leseni kwaajili yakuendesha shughuli zao kihalali huku wakitambulika na mamlaka husika kuwa niwafanyabiashara halali wa madini.
Mkuu wa Mkoa Gambo alimalizia kwakuwaadi kuendelea kukutana nao mara kwa mara angalau kila baada ya miezi mitatu na wafanyabiashara hao ilikufanya tathimini ya mambo mbalimbali ambayo wamekubaliana kama yatakuwa yamefanyiwa kazi na pia kama kutakuwa na mengine yaliyojitokeza.
Pia amewata wafanyabiashara hao wadogo wa madini kukaa pamoja na kamishina wa madini  wa kanda ili kuchagua uongozi wa mda wa chama chao kwakuwa uongozi uliopo ulionekana kutokubalika na wanachama  walio wengi, na uongozi huo utakuwa ukishughulikia matatizo na kero za wanachama wake kwa ukaribu zaidi.

Mmoja wa wafanyabiashara wadogo wa madini wa Jijini Arusha,Charles Liwa akizungumzia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika biashara yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Viongozi wengine wa Mkoa wa Arusha (hawapo pichani).

Wafanyabiashara wadogo wa madini wa Jijini Arusha wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,Arusha.

Monday, December 19, 2016

MAAGIZO YA MHE. WAZIRI MKUU KWA MKOA WA ARUSHA.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania,Kassim Majaliwa akisaini kitabi cha wageni cha ofisi ya mkuu wa mkoa,pembeni yake ni mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa maneno ya hitimisho ya ziara yake mkoani Arusha.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha,nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa waArusha.

MAAGIZO YA MHE.WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BAADA YA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA.

WATUMISHI WA UMMA

1.Watumishi wote wa umma wanapaswa kufanywa kazi kwauweredi,nidhamu na juhudi ili waweze kuwahudumia wananchi wananchi.

2.Ubaguzi katika kuhudumia wananchi ni mwiko, kila mwananchi anahaki yakupata huduma kwenye ofisi yoyote ya serikali.

3.Wakuu wa idara wasimamiemajukumuya idara zao kwakufuata ilani ya chama cha mapinduzi na pia maelekezo yaliyotolewa katika hotuba ya mhe. Rais wakati akihutubia bunge kwa mara ya kwanza.

4.Madeni ya watumishi yanayoweza kulipwa na Halmashauri yalipwe mapemaili kupunguza mlundikano wa madeni hku serikali inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi.

SEKTA YA ELIMU
I.Watoto wote wenye sifa yakuanza elimu ya awali waanze mara moja na wale waliofsulu kwenda sekondari, maafisa elimu wahakikishe wanajiunga na elimu ya sekondari bila kupoteza mda.

2.Ujenzi wa madarasa upewe kipaombele zaidi kwa wananchi kushirikishwa kwa wingi.

SEKTA YA AFYA

1.Kila kijiji kinatakiwa kuwa na zahanati na wananchi wahamasishwe kwenye ujenzi.

2.Serikali imetenga kiasi cha bil.1 kwaajiri ya manunuzi ya madawa kwa nchi nzima,mpaka sasa bil. 30 zimeshatolewa kwa manunuzi ya madawa hayo.

3.Wananchi waelimishwe na kuhamasishwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya.

SEKTA YA MIFUGO

1.Mifugo ya wenyeji itambuliwe na uongozi wa vijiji kwa kuwekewa alama ili kudhibiti ile inayotoka nje ya nchi.

2.Wananchi wenye mifugo mingi wanatakiwa kuipunguza ili waweze kuidumia vizuri nakujenga afya nzuri yakuweza kuuzika kwa bei nzuri.

SEKTA YA MALIASILI NA UTALII

1.Maeneo yote ya hifadhi yalindwe na kutunza kwa manufaa yakuongeza utalii nchini.

2.Mifugo inayoingizwa kwenye mbuga za wanyama iondolewe haraka.

3.Serikali ishirikiane na sekta binafsi waongeze nguvu katika kutunza utalii wa ndani hasa kwakuweka matangazo kwenye barabara za viwanja vya ndege hii itasaidia kukuza utalii wa ndani.

KILIMO
1.Wananchi wanatakiwa kuhamasishwa kulima mazao yanayostahimili ukame,hii itasaidia kuwa na chakula cha akiba kipindi cha ukame.

VIWANDA
1.Wawekezaji wamehamasishwa kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali hasa za utalii.

2.Wenye viwanda wameshauriwa kuendelea kulipa kodi na serikali haitamsamehe yoyote ambae atakwepa kodi.

NISHATI
1.Serikali imeshatenga kiasi cha trilioni 1 kwaajiri yakusambaza umeme katika vijiji vyote vilivyobaki havina umeme nchi nzima.

ZIARA YA KASSIM MAJALIWA WILAYANI ARUMERU

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizundua  jengo lenye madarasa mawili katika shule ya Sekondari Oljoro, wilayani Arumeru.

Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji katika  kijiji Oldenderet kata ya Nduruma, wilayani Arumeru.

Kassim Majaliwa akiongozana na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti kuelekea kwenye uwanja wa mkutano wa hadhara wa kijiji cha Oldenderet.

Kassim Majaliwa akiangalia ngoma kutoka katika kikundi cha utamaduni cha Oljoro.

KASSIM MAJALIWA AKIWA WILAYANI LONDIGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Londolwo wilayani Longido aliposimamaishwa njiani kujibu changamoto zao akielekea Longido na wakazi hao.

Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa mpaka wa Namanga(hawapo pichani) baada yakukagua kituo kipya cha forodha.

Wananchi wa Namanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wakumsikiliza Mhe. Kassim Majaliwa.

Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi wanaofanya kazi katika mpaka wa Namanga, wilayani Longido.

Waziri Mkuu Majaliwa ziarani Loliondo

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwasili wilayani Ngorongoro kuendelea na ziara yake katika Mkoa wa Arusha.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiangalia moja ya bidhaa za kitamaduni zilizotengeneza na wakinama wa Eminyatta,wilayani Ngorongoro.

Kassim Majaliwa akitoka katika moja ya nyumba za tamaduni za Eminyatta,katika kijiji cha Ololosokwani.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema sasa migogoro ya ardhi nchini ifikie mwisho kwa viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri kutafutia suluhu yakudumu katika maeneo yao.

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akimwagiza mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuitisha kikao maalumu cha utatuzi wa mgogoro wa ardhi uliopo katika kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro kati ya eneo la hifadhi na makazi ya watu ambao umedumu kwa mda mrefu.

“Namuagiza Mkuu wa Mkoa akishirikiana na mkuu wa wilaya ya Ngorongoro pamoja na kamati ya kijiji yakushughulikia migogoro ya ardhi na wawekezaji wakae wajadiliane namna yakupata muafaka wa mgogoro huu’.

Amesema ni vizuri wananchi nao wakashirikishwa pamoja na wawekezaji waliopo katika kijiji hicho ili maamuzi yatakayotolewa yawe shirikishi kwa pande zote.

Hata hivyo amewapongeza wananchi wa Ololosokwani kwakutambua umuhimu wakulinda na kuzithamini hifadhi za taifa na amewaadi kuwa serikali yao ipo pamoja nao katika kuunga mkono utunzaji huo wa hifadhi.

Amesisitiza zaidi kwa wananchi kulinda amani ya nchi yao kwa kuwatambua wageni wote wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu kusika na pale wanapowatilia mashaka watoe taarifa katika mamlaka husika na mifugo ya wenyeji ibainishwe haraka dhidi ya wageni.

Akifafanua ziadi Waziri wa maliasili na utalii Jumanne Maghembe amesema nivizuri mifugo yote ya wanakijiji cha Ololosokwan ikatambulika kwa kuwekewa alama ilikusaidia kubaini ile mifugo inayotoka nchi jirani nakuingia kinyemela.

Amesema ongezeko la mifugo hasa yakutoka nje ndio inayosababisha uvamizi wa maeneo ya hifadhi kwasababu wanakuwa wanatafuta maeneo ya malisho.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema tayari alishamuagiza mkuu wa wilaya ya Ngorongoro alipokuwa kwenye ziara yake kuunda kamati ndogo itakayofuatilia mgogoro huo na tayari kamati hiyo ilishaanza kazi ikiwa chini ya mkuu wa wilaya hiyo na ikimaliza kazi majibu yatapelekwa kwa wananchi.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa waso,Loliondo.




Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa amezipa miezi sita taasisi zisizo za kiserikali(NGO’s) zote za wilayani Ngorongoro kuhakikisha zinabadili mfumo wake wa utendaji kwakufuati usajiri.

Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa halmashauri ya Ngorongoro na baadhi ya viongozi wa NGO’s katika ukumbi wa halmashauri.

“Ninawapa miezi sita tu kwa NGO’s zote zilizopo wilayani hapa kuhakikisha zanabadili mfumo wake wa utendaji kwa kufuata shughuli walizosajiriwa nazo”.

Majaliwa amesema NGO’s nyingi hazifuati taratibu za utendaji kulingana na shughuli walizojisajiri, nyingi zimekuwa zikipata fedha kutoka kwa wafadhili na fedha hizo zinafanyiwa matumizi tofauti.

Pia amesema kuna baadhi yake zimefungua akaunti za benki nje ya nchi na fedha zote wanazopata kutoka kwa wafadhili zinawekwa huko wakati huo hazina akaunti yoyote kwa hapa nchini.

Majaliwa amesisitiza kuwa baada ya NGO’s zote kukamilisha zoezi hilo atamtuma mkaguzi mkuu wa hesabu wa serikali kuja wilayani Ngorongoro kukagua matumizi ya fedha zote zilizotumika tokea kila NGO ilipoanzishwa na ikibainika kulikuwa na udanganyifu zitafutiwa usajiri wake mala moja.

Hata hivyo Majaliwa ameshangazwa na wingi wa NGO’s zilizopo wilayani Ngorongoro ambazo ni zaidi ya 30 wakati kuna mikoa mingine inaitaji kuwa nazo lakini hakuna.