![]() |
Meneja wa Kampuni ya Milkcom maarufu Dar Fresh,Tunnu Mssika akimpa maelezo Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati akikagua mabanda ya waoneshaji bidhaa mbalimbali zinazotokana na Mifugo. |
RC Akiapishwa
Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.
Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania
Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.
JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja
Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha
Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Picha ya Pamoja
Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Thursday, May 31, 2018
MPINA AFUNGUA MAONESHO YA WIKI YA MAZIWA
Wednesday, May 16, 2018
VITUO VYA AFYA KUJENGWA LONGIDO
By TAARIFA ZA ARUSHA May 16, 2018
Afya, Arusha, Habari, Maisha, Matukio, Miundombinu, Uchumi No comments
Monday, May 14, 2018
LONGIDO YAPATIWA SIKU 7 KUJIBU HOJA ZA CAG
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo akimchukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada ya kutoa maelekezo ya namna ya kujibu hoja za CAG. |
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Longido alipokuwa akuzungumzia hoja za CAG. |
Friday, April 27, 2018
KATIBU TAWALA AKUTANA NA WAJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA
By TAARIFA ZA ARUSHA April 27, 2018
Afya, Arusha, Elimu, Habari, Matukio, Miundombinu, Uchumi, Utalii No comments
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega, akiwa na wajumbe kutoka Benki ya Dunia ofisini kwake pamoja na wataalamu kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Arusha. |
Katibu Tawala Bwana Richard Kwitega,akiongoza kikao kilichowakutanisha ujumbe kutoka Benki ya Dunia na wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Arusha. |
UZINDUZI WA CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Ushirikishwaji katika kutoa chanjo ya saratani ya mlango
wa kizazi kutoka katika sekta mbalimbali hasa za dini,kisiasa na kabila ni
muhimu sana.
Akiyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amesema kuwa zoezi hili lisichanganywe na
mambo ya siasa bali sekta hizo zitumike kutoa elimu zaidi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizindua utoaji wa chanjo hiyo
kimkoa katika shule ya msingi Ngarenaro,ambapo amesema wasichana 21,198
watapatiwa chanjo hiyo kwa mkoa wa Arusha.
Aidha,saratani ya mlango wa kizazi niya pili baada ya
saratani ya matati, kwa asilimia 38 na niya kwanza kwakuwa na vifo vingi kwa
Tanzania, ikifuatiwa na saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia 32.8,saratani
ya koo asilimia 10.9 na saratani ya tezi dume kwa asilimia 2.1.
Chanjo hii inapatikana katika vituo vyote vya afya na ni
bure kwa wasichana wenye umri wa miaka 14.Kila mwaka wanawake 466,000
wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi.
Akizungumza kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa wa
Arusha,mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Vivia Tomothy Wonanji, amesema kila mtoto
aliyefikisha miaka 14 anatakiwa kupatiwa chanjo hii na itarudiwa baada ya miezi
sita ya chanjo ya kwanza.
Amewashukuru wadau wote walioshirikiana na Serikali
katika kufanikisha upatikanaji wa chanjo hii na bure nchi nzima.
Amewatoa shaka wananchi wote kuwa chanjo hiyo ni salama
kabisa na elimu itaendelea kutolewa kwa watu ili kuwaondoa wasiwasi wakuwa
chanjo hii inaharibu kizazi.
Chanjo hii yakuzuia saratani ya mlango wa kizazi
ilizunduliwa hivi karibuni nchini na waziri wa afya,maendeleo ya jamii, jinsia,
wazee na watoto Ummi Mwalimu na kufuatia uzinduzi mdogo katika mikoa na
halmashauri zote ambapo kwa Arusha ilizinduliwa mnamo Aprili 25,2018.



















