RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Tuesday, December 6, 2016

WAZIRI MKUU WILAYANI KARATU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisoma mabango ya wananchi wa kijiji cha Qandged wilayani Karatu baada yakufunga njia kuzuia msafara wake usipite.

Kassim Majaliwa akikagua mfereji wa maji uliojengwa na World Vision unaopeleka maji kwenye kisima katika kijiji cha Jobaj.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo kuondoa mashine zakupampu maji zilizowekwa kwenye chanzo cha maji cha kijiji cha Qangded kata ya Eyasi wilayani Karatu.
 Akitoa maelekezo hayo Majaliwa wakati  alipokuwa anaongea na wanakijiji wa Jobaj katika mkutano wa hadhara ambapo alizindua kisima cha maji.

Alisema mashine hizo zimekuwa zikitumika kunyeshea mashamba ya wafanyabiashara  wakubwa wa vitunguu na mahindi nakusababisha kasi ya maji kwenye mifereji kupungua nakupelekea wakazi wengi wa kijiji hicho kukosa maji kwa mda mrefu.


“Baada ya siku moja Mkuu wa wilaya apite kukagua na akikuta bado mashine hizo zipo azikamate nakuwachukulia hatua kali wahusika kwakuwa wanaharibu vyanzo vya maji”. Alisema.

Pia amewataka wananchi wote kuwa walinzi wa vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo yao na watoe taarifa mapema kwa mamlaka husika pale wanapogundua kuna uharibifu umefanyika.

Wananchi wanatakiwa kufuata sheria yakutofanya shughuli zozote za uzalishaji ndani ya mita 500 kutoka katika vyanzo vya maji na waliofanya hivyo waondolewe mara moja.

Majaliwa amelipongeza shirika la World Vision Karatu kwakujenga mifereji yakutoa maji kwenye chanzo  cha maji hadi kwenye visima ambavyo wananchi wanapata maji,hizo ni juhudi kubwa zilizofanywa na shirika hilo na serikali inatambua mchango wao huo mkubwa.

Amewata mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kujenga utamaduni wakusiliza kero mbalimbali za wananchi nakuzichukulia hatua mara moja.

Waziri Mkuu Majaliwa akiangalia naoma maji yanavyokusanywa kwenye mrefeji kabla yakuelekezwa kwenda kwenye kisima cha kijiji cha Jobaj

Majaliwa akikagua moja ya shamba lililolimwa kutokana na kilimo cha umwagiliaji cha kijiji cha Qandged wilayani Karatu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia kwake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakikata utepe kama ishara yauzinduzi wa kisima cha maji cha kijiji cha Jobaj wilayani Karatu.

Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa(MB) akuzungumza na wananchi wa Karatu katika uwanja wa Baraa Karatu Mjini baada yakumaliza ziara wilayani humo.






Monday, December 5, 2016

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA MKOANI ARUSHA

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa,akiwasalimia wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Mkoa Mt. Meru.

Waziri Mkuu Majaliwa azuru kabuli la merehemu Edward Moringe Sokoine, wilayani Monduli.

Mhe.Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Emeirete wilayani Monduli.

Kassim Majaliwa azindua wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Monduli.




Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa amewataka watumishi wote wa serikali kuzingatia uwadilifu,uwaminifu na uwajibikaji katika utendaji wao wa kazi.

Ameyasema hayo alipokuwa akuzungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada yakufungua wodi ya mama wajawazito ya hospitali ya wilaya ya Monduli.

“Serikali ya awamu ya tano niyawawajibikaji,waadilifu katika sekta za umma”,alisema Majaliwa.

Amewataka watumishi wawasikilize,wawahudumie na kuwatumikia wananchi bila yakuweka ubaguzi wa aina yoyote ile.

Hii itasaidia kuonyesha matokea bora ya kila mtumishi kulingana na taaluma aliyonayo nakupelekea kuongeza ufanisi zaidi serikalini.

Aidha amewataka viongozi wa halmashauri kusimamia fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa na serikali na zikafanye shughuli ambazo zilipangiwa.

Kila sekta katika halmashauri ihakikishe inapanga majukumu yake nakuyatekeleza kadri inavyopaswa.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa mto wa Mbu wilayani Monduli.


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ha Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa amekonga nyoyo za wakazi wa Monduli kwakuwakabidhi hati ya shamba la Manyara Ranch yenye jina la halmashauri ya Monduli.

Akikabidhi hati hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Monduli Steven  Ulaya amesema shamba hilo lilikuwa kilio cha mda mrefu kwa wakazi wa Monduli hususani wanakijiji cha Isilarei na Olutukai.

Ambao ndio wamiliki halali wa shamba hilo chini ya halmashauri ya Monduli lakini lilimilikishwa kwa taasisi ya TCLT (Tanzania Land Conservation Trust) kimakosa.

“Nawakabidhi hati hii ya shamba yenye jina la halmashauri kama msimamizi wa shamba hili kwaniaba ya wananchi wa vijiji vya Isilarei na Olutukai”.

Shamba hili lilikuwa linamilikiwa na taasisi ya TCLT kwaniaba ya halmashauri lakini serikali ya Mkoa wa Arusha kupitia Mkuu wa Mkoa wake Mrisho Mashaka Gambo aliagiza halmashauri ya wilaya ya Monduli kuhakikisha hati hiyo inarudishwa chini ya halmashauri.

Ndani ya wiki moja tayari halmashauri ikawa imefanya maamuzi yakubadili kwakufuata taratibu zote zakubadili jina la umiliki kutoka TCLT nakusomeka halmashauri ya wilaya ya Monduli amboa ndio wamiliki halali wa shamba hilo.

Shamba hilo sasa lipo chini ya halmashauri ya wilaya ya Monduli na wanakijiji wa vijiji hivyo wanaruhusiwa kutumia ardhi hiyo kwakufuata taratibu kwa shughuli za maendeleo yao.

Mheshimiwa Majaliwa alikuwa na ziara ya siku moja katika wilaya ya Monduli na ataendelea na ziara yake katika Mkoa wa Arusha  kwenye wilaya ya Karatu na kisha Ngorongoro.

ZIARA YA WAZIRI MKUU JIJINI ARUSHA

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha Lodhia Industries,Njiro.

Kassim Majaliwa akielekezwa shughuli za uzalishaji mali katika kiwanda cha Hans Paul,Njiro.

Waziri Mkuu akimkabidhi madawati 1000 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Gambo yaliyotengenezwa na kiwanda cha Fibre board,Njiro

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa jiji la Arusha katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid,Arusha.

Kassim Majaliwa akimkabidhi funguo za pikipiki mmoja wa waendesha bodaboda wa jiji la Arusha.

Hizi ni pikipiki 200 alizozikabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa waendesha bodaboda,Jijini Arusha

Hili ni vazi rasmi la wazawa wa mkoa wa Arusha(wamasai),Majaliwa akiwa amevalishwa kumpa heshima kubwa kama mmoja wa viongozi wa kabila la hilo.

Saturday, December 3, 2016

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA JIJI LA ARUSHA.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara wa Jiji la Arusha katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha.  




Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Mjaliwa amewata wafanyabiashara kuwekeza zaidi kwenye sekta mbalimbali hasa za viwanda hapa nchini.

Aliyasema hayo alipokutana na wafanyabiashara wa jiji la Arusha nakuwashauri wawekeze kwenye mikoa yote ya Tanzania hasa kwakuanzisha viwanda,ilikujenga nchi ya viwanda kama dhamira ya serikali ilivyo.

“Nawashuri muwekeze kwenye mikoa yote hapa nchini na niruksa kabisa viwanda vingi vianzishwe”.

Hata hivyo amewata waendelee  kushirikiana na serikali yao ya awamu ya tano kwakuwa ipo pamoja nao na inaongeza ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wote nchini ili wawe na amani na waweze kuwekeza zaidi.

Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha zaidi kwenye sekta binafsi hasa kwakupambana na wasiolipa kodi ili walipe nakuweka usawa katika biashara na kukuza ushindaji wa biashara.

Aidha Majaliwa amewataka watendaji wa serikali kuvilinda viwanda vya ndani kwakuhamasisha matumizi  ya rasilimali za ndani napia kuzipunguzia ushuru ili viwanda viweze kukuwa kwa kasi kama serikali inavyodhamiria kujenga nchi ya viwanda.

Majaliwa bado anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa kutembelea halmashauri zote za Mkoa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(Kulia) na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laiza, katika mkutano na wafanyabaishara wa jiji la Arusha.