RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Wednesday, July 12, 2017

KATIBU TAWALA,RICHARD KWITEGA ATEMBELEA KITUO CHA SOS CHILDREN VILLAGE

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega, akiwa pamoja na baadhi ya vijana wanaolelewa katika kituo cha SOS Children Village tokea wakiwa na umri wa miaka 3 na baadhi ya walezi wao,Ngaramtoni.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega amesema serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wa karibu sana  na taasisi ya SOS Children Village kwenye shughuli wanazofanya hususani zakusaidia watoto wasio na wazazi.

Aliyasema hayo alipotembelea kituo hicho kwa lengo lakutaka kufahamu zaidi namna taasisi hiyo inavyofanya kazi ilikuona nikwajinsi gani serikali inaweza kushirikiana nayo katika kuwalea watoto hao kwakuwa na wao niwatanzania wanahaki zote zakuhudumiwa na serikali yao.

“Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi hii katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma iliyo bora kwa watoto wetu hawa na wao waweze kujisikia kweli serikali yao ipo pamoja nao.”

Aidha, amepongeza taasisi hiyo kwa kutoa malezi mazuri kwa watoto hao hasa kwakuwalea kama wapo na wazazi wao halisi hasa kwakuwapa elimu na huduma ya afya.

Bwana Kwitega amesisitiza zaidi kuwa serikali kwa kuanza inaweza kutoa ushirikiano kwa kuleta wataalamu wa elimu yani walimu na wataalamu wa afya ambao watakuwa waajiriwa wa serikali lakini wakitoa huduma katika kituo hicho.

Akitoa historia fupi ya taasisi hiyo,Mkurugenzi wa taasisi hiyo bwana Francis Msollo alisema kituo hicho kilianza mwaka 2000 kikiwa na nyumba 10 tu zakuishi watoto hao lakini mpaka sasa wamefikisha nyumba 15 na watoto 200.

Pia alisema mbali yakuwalewa watoto hao wasio na wazazi, taasisi inatoa pia msaada kwa wale watoto wenye mzazi mmoja kwakuwapa ufadhiri wa elimu inayotolewa katika taasisi hiyo.

Taasisi hiyo pia imetoa nafasi kwa watoto wanaozunguka maeneo ya taasisi hiyo kupata elimu inayotolewa katika kituo hicho.

Akisisitiza zaidi bwana Msollo alisema, Changamoto wanayokabilina nayo kwasasa nikwabaadhi ya wafadhili kujitoa katika kutoa fedha zakutoa huduma za afya na elimu na hivyo kuiomba serikali iangalie naoma yakusaidia taasisi hiyo ili watoto hao waendelee kupata elimu bora na afya.

Msollo amesema, mipango ya baadae ya taasisi hiyo nikuboresha mabweni ya watoto hao iliwaweze kuchukua watoto wengi zaidi wakiwemo watoto wa mbali na mazingira hayo, pia usafiri kwa watoto hao wanaotoka mbali huku elimu itolewe zaidi katika jamii juu yakuwahudumia watoto hao yatima katika maeneo yao.

Taasisi ya SOS Children Village iliaanzishwa mwaka 1984 huko Zanzibar na baadae kufungua vituo vingine vinne katika mikoa ya Mwanza,Dar es Salaam, Arusha na Iringa, hadi sasa imeshaeenea katika nchi mbalimbali kama South Afrika na Uganda.




Katibu Tawala Richard Kwitega, akimsikiliza mmoja wa vijana aliyelelewa na kituo cha SOS Children Village Bi. Anna Lomayani na sasa anafamilia yake.

Bwana Kwitega, akiwasalimia baadhi ya watoto wa shule ya awali wa kituo cha SOS Children Village.

Thursday, July 6, 2017

MAONYESHO YA NANE NANE 2017.

Katibu Tawala akitoa maelezo juu ya maadhimisho ya siku ya nane nane kwa kanda ya Kaskazini.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard  Kwitega amesema kuwa maonyesho ya wakulima maarufu kama nane nane ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja wa Themi Njiro yataendelea kuwepo kama kawaida.

Ameyasema hayo baada yakutokea sitofahamu kwa wananchi kutokana na iliyokuwa taasisi yakusimamia maonyesho hayo (TASO) kuzuiliwa kuendelea kuratibu maonyesho hayo.

Aidha, amesema kwa mwaka huu maonyesho hayo yataratibiwa kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Sekretarieti za Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara pamoja na TASO.

Hata hivyo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ikiwa ndio mwenyeji wa maonyesho hayo ndio imepewa jukumu lakusimamia uwandaaji wa shughuli zote katika viwanja hivyo.

Ametoa wito kwa washiriki wote wa maonyesho hayo kwa mwaka huu  2017 kuanza maandalizi mapema ikiwemo ulipaji wa ada ya ushiriki katika ofisi zilizokuwa za TASO ndani ya viwanja vya nane nane ambapo kwa sasa kuna maafisa walioteuliwa kutoka katika Wizara na Sekretarieti ya Mkoa kutumia ofisi hizo kwa shughuli hizo.

Pia shughuli nyingine za Maandalizi zikiwemo kuwasilisha mahitaji ya idadi ya waoneshaji, Magari, na taarifa nyingine zifanyike katika ofisi za TASO kabla ya Julai 20,2017.

Kwa mwaka huu maonyesho hayo yatabeba kauli mbiu isemayo “Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”,ambayo yataanza rasmi Agosti moja,2017 nakumalizika Agosti 10,2017.

TANGAZO KWA WANANCHI WOTE


Saturday, July 1, 2017

Wadau wa maendeleo ya vijana mkoani Arusha wahaswa kushirikiana na serikali

Baadhi ya wadau wa maendeleo ya vijana waliohudhuria kikoa na serikali ya mkoa wa Arusha, wakisoma taarifa zakutoka serikalini.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akiwa na baadhi ya viongozi wa taasisi za maendeleo ya vijana, kutoka kulia ni Mkurugenzi kutoka VETA Mr. Mrefu na kushoto ni Vicent Buhega wa Voice of Youth Tanzania.


Taasisi binafsi zinashughulika na maendeleo ya vijana jijini Arusha zimehaswa kuhakikisha zinashirikiana kwa kiasi kikubwa na serikali katika kuweka wazi shughuli zao wanazofanya katika Mkoa wa Arusha.

Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana kwa mkoa wa Arusha, kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkoa.

“Nafahamu kuwa taasisi hizi binafsi sio adui wa serikali kilichopo ni kulikuwa na mahusiano ya mbali kati yenu na serikali, serikali ilikuwa haitambui shughuli zenu na nyinyi mlikuwa hamfahamu serikali yenu inaitaji nini”.

Gambo amesisizaidi kwa taasisi hizo kuhakikisha zinafanya kazi ambazo ni hitaji kubwa kwa vijana wetu badala yakutekeleza matakwa ya wafadhiri wao tu.

Amesema lengo kubwa lakukutanisha taasisi hizo na serikali nikufahamiana na pia kuweka mikakati ambayo itaenda sambamba na serikali ya awamu ya tano ambayo inapiga vita madawa ya kulevywa,mimba za utoto na utegemezi.

Hivyo amezitaka taasisi hizo za maendeleo ya vijana kuhakikisha zinatoa elimu yakutosha ya afya ya uzazi kwa vijana,madhara ya madawa ya kulevywa na elimu ya ujasiliamali, ili vijana waweze kujikwamua katika maisha kwakufanya kazi kwa bidii.

Aidha, amezitaka taasisi hizo kuzitambua fursa zilizopo serikalini kama za mikopo kutoka mfuko wa taifa wa maendeleo ya vijana na asilimia 5 ya mapato kutoka katika kila halmashauri ambazo zinapelekwa kwa vijana.

Hivyo taasisi hizo zinatakiwa kuweka utaratibu wakuisaidia serikali katika kuzisimamia fedha hizo ili ziweze kuwanufaisha vijana kwa kiasi kikubwa na wao wakiendelea kuwapa mafunzo zaidi ya ujasiliamali ikiwemo uwandikaji wa miradi mbalimbali.

Kikao hicho kimefanyika kwa mara ya kwanza kwa mkoa wa Arusha kwa lengo lakufufua mahusiano ya karibu baina ya serikali na taasisi zinashughulika na maendeleo ya vijana na moja ya makubalino waliyoafikiana nikuandaa kongamano la vijana kimkoa na kamati mbalimbali zimeundwa zakusimamia muendelezo wa vikao vijavyo.

Thursday, June 22, 2017

Halmashauri za mkoa wa Arusha zahamasishwa kutenga maeneo ya viwanda.

Baadhi ya viongozi kutoka katika halmashauri za mkoa wa Arusha waliohudhulia kikao cha mipango mikakati cha halmashauri.  


Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha zimehamasishwa kutenga maeneo maalumu kwaajili ya ujenzi wa viwanda kama maelekezo ya serikali ya awamu ya tano yanavyoelekeza.

Ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na viongozi wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha kwa lengo lakuweka mikakati yakiuntendaji hasa kwa mwaka wa fedha unaokuja 2017/2018.

“Nazitaka halmashauri zote zieleze hapa namna zilivyojipanga kwa mwaka wa fedha ujao katika kutekeleza adhima ya serikali ya viwanda,bainisheni maeneo mliyotenga na muelezee hali ya miundo mbinu ya msingi ilivyo,lina ukubwa gani,lina hati au halina hati na niaina gani ya kiwanda mmependekeza.”

Aidha amewata watumishi wote wa serikali kubadilika kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake kila mtu afanye kazi kwa bidii hasa kwakutekeza malengo ya serikali.

Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote ambae atakwamisha malengo ya serikali hivyo hatua zakitumishi zitatumika kwa mtumishi huyo ili kukuza ufanisi sehemu za kazi.

Gambo anaendesha kikao cha siku 3 kwa kupitia mipango mbalimbali yakila halmashauri nakushauri nini kifanyike kwa mwaka wa fedha ujao.

Friday, May 5, 2017

RC GAMBO AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI WA MKOA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha mrisho Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakisiliza mafunzo elekezi ya viongozi wa mkoa wa Arusha.     


Viongozi wa Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuwajibika katika majukumu yao huku wakifuata kanuni na sheria mbalimbali za utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi huku wakileta maendeleo kwa mkoa.

Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi hao  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema viongozi wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuongeze mahusiano katika maeneo yao ya kazi baina yao na watumishi wachini yao.

Amesema lengo kubwa nikuondoa migongano inayojitokeza baina ya viongozi na watumishi hao ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji  wa kazi katika maeneo yao na kuongezeka wimbi la uwonevu kwa watumishi wao.

Aidha amewataka viongozi hao wasimamie uwajibikaji wa watumishi katika maeneo ya kazi kwa kufuata taratibu za majukumu yao.

Akisisitiza zaidi kwa kuwataka viongozi kutekeleza maelekezo yanayotolewa na ngazi za juu serikalini kwani mengi yanakuwa ni miongoni mwa shughuli zao za kila siku na hii itaongeza utii kwa viongozi serikalini.

Nae katibu tawala wa mkoa  Richard  Kwitega amesema mafunzo hayo niyakukumbushana majukumu kwa viongozi hao huku wakipitia maeneo mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya viongozi,usimamizi wa Rasilimali watu sehemu za kazi napia kupitia kanuni na maadili ya viongozi na utumishi wa umma.

Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 2 huku yakishirikisha baadhi ya viongozi kutoka TAMISEMI.

Mkuu  wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta wakisikiliza mafunzo ya viongozi wa Mkoa wa Arusha yaliyotolewa kwa lengo lakukuza uwelewa.

Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo elekezi kwa viongozi wa mkoa wa Arusha.

WAZIRI MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA TENGERU SAKINA

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akitoa malekezo kwa viongozi wa mkoa wa Arusha alipokuwa akikagua barabara inayojengwa ya Tengeru  mpaka Sakina, jijini Arusha.

Mhe.Kassim Majaliwa akiwa pamoja na viongozi wa Mkoa wakikagua barabara inayojengwa ya Tengeru mpaka Sakina,Jijini Arusha.

Wednesday, May 3, 2017

Tangazo la kuripoti kazini kwa madaktari wote wapya


Monday, April 10, 2017

Wafanyabiashara Arusha wafarijika na maelekezo ya RC Gambo