RC Akiapishwa

Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Mhe. Mrisho Gambo.

Ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa Ofisini kwake, Jijini Arusha.

JPM ,Mrisho Gambo Picha ya Pamoja

Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Samia Suluhu Hassan akiwasili Jijini Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mhe Mrisho Gambo Akimpokea Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Picha ya Pamoja

Mhe. Mrisho Gambo akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.

Friday, September 30, 2016

VIFUNGASHIO BORA VYA MIPIRA YA KIUME

Muuguzi Mkuu  Mkoa wa Arusha, Bi. Mwamini Juma Nyakwela, amezindua rasmi mpira wa kiume (Kondom),unaoitwa ZANA kwa mikoa ya Manyara na Arusha ambayo ipo katika kifungashio kipya,uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha mafunzo ya afya(CEDHA) Jijini Arusha.
Uzinduzi huo umefanyika baada ya mipira hiyo kuwekwa katika vifungashio vipya na hivyo kubadili muonekano uliokuwa umezoeleka  zamani.
 “Leo hii tunazindua mipira hii yakiume ambayo imebadilishwa kifungashio lakini ubora wake uko pale pale,watu endeleeni kuitumia,”amesema.
 Watu wengi waliaacha kutumia mipira hii kwasababu haikuwa kwenye vifungashio vizuri na wakawa wanatumia aina nyingine ,lakini kwasababu Serikali inawajali wananchi wake ikaamua kubadili vifungashio ili wananchi waendelee kuzitumia zaidi.
Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa zilionyesha  asilimia 69 ya wanawake na asilimia 77 ya wanaume wanauelewa mzuri juu ya matumizi sahihi ya mipira ya kiume lakini ni asilimia 27 tu ndio wametumia mipira hii.
Aidha Kaimu Mkuu wa kitengo cha Elimu,Habari na Mawasiliano kwa mpango waTaifa wa kudhibiti UKIMWI kutoka Wizara ya fya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Edda Katikiro,amesema mipira hii ya jina la ZANA imeshasambazwa rasmi  kuanzia Juni 2016 na zilitengenezwa takribani  Milioni 21 lakini bado Wizara inaendelea kutengeneza nyingine zaidi.
Akisisitiza zaidi juu ya mipira hii yenye vifungashio vipya,amesema wananchi hawanabudi sasa watumie hii mipira kwasababu hakuna kilichobadilika zaidi ya kifungashio tu, na Serikali inatoa bure kwa nchi nzima.
“Hii ni ileile mipira ya kiume iliyokuwa inatumika tokea zamani mabadiliko haya ya vifungashio yasiwaogopeshe watu wakajua ni mipira mipya,”alisisitiza Edda.
Kutokana na dhana potofu iliyokuwepo katika jamii juu ya muonekana ambao haukuwa mzuri kwa hii mipira ya kiume hususani huko nyuma ikapalekea watu wengi kutoziamini kwa ubora wake na hata wengine kutozitumia kabisa.
Aidha amewata watu wajitaidi kupata elimu sahihi juu ya matumizi ya mipira hii, ilikupunguza au  ikiwezekana kutokomeza kabisa magongwa ya zinaa,UKIMWI na mimba zisizotarajiwa.
Kwa Mkoa wa Arusha maambukizi ya UKIMWI kwa mwaka 2016 ni asilimia 3.2 kulinganisha ni kiwango cha Taifa cha asilimia 5.1, hivyo kwa Mkoa kasi ya maambukizi ipo chini,na usambazaji wa mipira ya kiume tayari Mkoa ulishapeleka maombi yake nakupatiwa mipira hii aina ya ZANA na imeshasambazwa katika vituo vyote vya afya.
Uzinduzi kama huu umeshafanyika katika mikoa ya Mbeya na Mwanza na utaendelea zaidi kwa mikoa mingine na juhudi kubwa imeshawekwa kwa upande wa Serikali katika kuhakikisha mipira hii inatumika kwa kiasi kikubwa ili kufikia mwaka 2020 UKIMWI uwe umetokomezwa kabisa na wadau mbalimbali wazidi kushirikiana na Serikali katika mapambano hayo.





Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Elimu,Habari na Mawasiliano katika Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Bi.Edda Kitiro,akitoa historia fupi ya sababu iliyopelekea kubadili vifungashio vya mipira ya kiume, kwa washiriki walioshiri uzinduzi wa mipira hiyo, Mkoani Arusha.

Hawa ni baadhi ya washiriki walioshiriki uzinduzi wa mipira ya kiume,wakifuraia muonekao mpya ya mipira hiyo,Jijini Arusha.

Huu ni muonekana mpya wa mipira ya kiume,ambao umezinduliwa rasmi kwa mikoa ya Arusha na Manyara.

Thursday, September 29, 2016

MRISHO GAMBO AFUNGUA MKUTANO WA WAFAMASIA.

Mkuu wa Mkoa,Mrisho Gambo akifungua mkutano wa mafamasia,uliofanyika katika ukumbi wa Naura,Jiji Arusha.

Rais wa chama cha wafamasia(PST) Michael  Kishiwa ,akielezea historia fupi ya chama chao kwa mgeni rasmi,ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.

Baadhi ya wafamasia waliokuwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa(hayupo pichani)alipokuwa akifungua mkutano wa chama cha wafamasia,Jiji Arusha.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa chama cha wafamasia(PST),Naura Jijini Arusha.

Friday, September 23, 2016

Wadau wa Sekta ya Utalii Mkoani Arusha kunufaika zaidi.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,ameongoza mkutano mkuu wa wadau wa utalii wa Mkoa wa Arusha ambao umefanyika katika ukumbi wa AICC Arusha. Ambapo mambo mbalimbali yamejadiliwa kuhusu sekta hii ya utalii na kuangalia jinsi yakuikuza zaidi kwa miaka ya mbeleni.

Akizungumza na wadau hao alisema sekta hii ina changamoto mbalimbali zikiwemo za ongezeko la kodi ya utalii pamoja na kadi nyingine ndogondogo wanazotozwa pindi wakiwa na wageni wao.

“Najua wafanyabiashara wengi hapa wametishika sana nah ii kodi ya utalii ilioanza kutozwa hivi karibuni nakuwafanya muone kuwa biashara zenu zimeanza kuyumba kwa watalii kutotaka kufika tena nchini.”

Alisistiza kuwa kuna fursa mbalimbali katika sekta hii ya utalii ambazo zinaweza kukuza zaidi biashara hii nakuwavutia zaidi wageni kutoka nje napia ushirikishwaji wa wadau wa utalii na Serikali ni kitu chamuhimu sana ndio maana nimeamua kuandaa huu mkutano ili tuweze kuanzimia mambo mbalimbali kwa pamoja.

Akituoa ufafanuzi wa kodi wa utalii iliyoanza kutumika Julai 1,2016 mpaka Agosti 2016 ,Mkuu wa Kitengo cha elimu na mapato Euginia Mkumbo ,amesem kuna ongezeko la kodi kwa  kiasi cha  bilioni 5.8 ambayo ni asilimia 120 kutoka kwenye kodi za hoteli na utalii wakati  mwaka jana ilikuwa bilioni 2.5 kutoka kwenye kodi za hoteli tu.

Aidha ongezeko hilo la kodi ya utalii imeonyesha kunaongezeko kubwa la mapato yaliyoingia Serikalini na wakati huo wageni wengi hawajapatwa na usumbufu wowote tokea kodi hii ya utalii ilipoanza kutumia.

Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators (TATO) bwana Wilbad Chambulo,amesema kuanzishwa kwa kodi hiyo ya utalii kwa upande wao haina shida isipokuwa hawakupewa taarifa mapema na taasisi husika iliwaweze kujipanga.

Kwetu sisi hii kodi haina shida ila tatizo ni taarifa zimetufikia kwa gafla sana nakutufanya tukose mda wakujianda,”alisema Chambulo.

Pia  alilisitiza kwa Serikali kusimamia sheria zaidi ili wafanyabiashara wote wa sekta  waweze kulipa kodi  kuliko kwa sasa ni baadhi yao tu ndio wanalipa na wengine hawalipi.

Aidha aliomba utaratibu wa malipo kwa taasisi husika uwangaliwe upya kwani kwa sasa unamlolongo mrefu sana unaopelekea kuwachukua mda mrefu sana pindi wanapoenda kufanya malipo hayo au kodi zote zingewekwa kwenye fungu moja iliziweze kulipwa kwa mala moja.

Mambo mbalimbali yameathimiwa katika mkutano huo ikiwemo kuimalisha ulinzi na usalama kwa watalii wote watakaoingia mkoani na pia litaanzishwa dawati maalumu lakusikiliza Changamoto mbalimbali zitakazo kuwa zinawakabiri wadau hao wa utalii nakuzitafutia ufumbuzi kwa haraka.


Mwenyekiti wa TATO Wilbad Chambulo akizunguza kwenye mkutano wa wadau wa utalii uliofanyika katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha.
Baadhi ya wadau wa utalii waliohuzulia ukutano wa wadau wa utalii ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa,jijini Arusha.

MKOA WA ARUSHA KUNUFAIKA NA UWEKEZAJI KUTOKA CHINA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka  nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake.

Amewahakikishia kuwapa ushirikiano,mazingiza mazuri  na usalama kwa wawekezaji kutoka China watakaofika kuwekeza katika Mkoa wa Arusha, na watakapoitaji msaada wowote kutoka Serikalini basi watapatiwa kwa wakati.

“Kwa Mkoa wa Arusha mtapata ushirikiano wakutosha kutoka Serikali na mtakapoitaji msaada sehemu yoyote katika utendaji wenu wa kazi basi msisite kuwasiliana nasi na tutawasaidi”,alisema Gambo.                                                     

Aidha mjumbe kutoka ubalozi wa China kwa Tanzani bwana Gou Huodong,amemwakikishia Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwa ataenda kuwahamasisha wachina wengine waliopo China kuja kuwekeza zaidi Mkoani Arusha hasa kwenye sekta ya Utalii ambayo ndio inayokuwa kwa kasi sana na inaongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa.

“Nitaenda  kuwahamasisha wenzangu huko China waje kwa wengi hapa Mkoani Arusha kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbalia hasa ya Utalii kwasababu sekta hii inakuwa kwa kasi sasa,”alisema Gou.

Pia Muheshimiwa Gambo aliwaelezea mpango wakufunga Kamera za barabarani(CCTV) kwa Mkoa wa Arusha ilikuimalisha zaidi ulinzi na Usalama hasa kwa wawekezaji na watalii wanaoingia katika Mkoa huu, na hivyo kuwaomba waangalie hiyo fursa kwa upande wao iliwaisaidie Serikali katika kuimalisha ulinzi wake maeneo mbalimbali ya Mkoa.


Ugeni huu kutoka ubalozi wa China hapa nchini ulikuwa na lengo kubwa lakuweza kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo katika Mkoa wa Arusha, kwakuwa wageni wengi kutoka China waliofika katika Mkoa wa Arusha walikutana na mazingira mazuri ya uwekezaji.


Mjumbe kutoka ubalozi wa China nchini Gou Huodong,akielelezea jinsi atakavyowahamasisha wawekezaji wengi kutoka China waje kuwekeza Mkoani Arusha,pembeni ni Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akipeana mkono kama ishara ya ushirikiano baina ya nchi ya China na Mkoa wa Arusha na Mjumbe kutoka ubalozi wa China Nchini Gou Huodong.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe kutoka nchini China na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha,nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Wednesday, September 21, 2016

MKUTANO WA WADAU WA UTALII KUFANYIKA MKOANI ARUSHA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akizungumza na waandishi wa habari wa Arusha,akiwaelezea juu ya mkutano mkuu wa wadau wa Utalii utakaofanyika Septemba 22,2016 katika ukumbi wa Mbayuwayu (AICC).

WALIMU WA JIJI LA ARUSHA WANEEMEKA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza na walimu wa shule za Msingi na Sekondari za Jiji la Arusha,katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Hawa ni baadhi ya walimu wa shule za Msingi na Sekindari wa Jiji la Arusha waliokuwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani)alipozungumza nao.

MAKAMU WA RAIS,SAMIA SULUHU HASSAN KUFUNGUA MKUTANO WA SARPOCCO JIJI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili uwanja wa ndege wa Kitaifa wa Kilimanjaro(KIA),kwaajiri yakufungua mkutano wa SARPOCCO EXTRA ORDINARY MEETING,utakaofanyika  Septemba 16,2016 katika ukumbi wa AICC.





Friday, September 16, 2016

MKUU WA MKOA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UTUME WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO


  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akiongozwa na vijana wa Skauti kwenda kukagua mabanda ya taasisi za kanisa la waadventista wa Sabato Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  akikagua mabanda yenye vitabu na majarida mbalimbali yanayochapishwa na taasisi za kanisa la wasabato Tanzania,kushoto ni Mchungaji Eliasi Ijiko.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akikata utepe kama ishara ya maadhimisho ya maiaka 50 ya Utume Burka,kushoto ni Mch. Mchungaji Eliasi Ijiko na kulia ni Askofu Godwin Godwin Lekundayo

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akisoma  hotuba yake kwa viongozi na waumini wa waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(katikati) na viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika picha ya pamoja.
Viongozi wa dini nchini wameombwa kuhamasisha waumini wao kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo katika Taifa la Tanzania na pia wametakiwa kuhamasisha waumini wao kuhakikisha wanadai risiti kila wanapoenda kununua bidhaa au  kupata huduma mbalimbali.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr John Joseph Pombe Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.

Akizungumza na waumini na viongozi wa Kanisa hilo lililopo Burka mjini hapa, Mkuu wa Mkoa Arusha Gambo alisema, Watanzania wanalojukumu la kufanya kazi kwani hata  Vitabu vya Dini vimeelekeza kuwa mtu asiyefanya kazi na asile na mafundisho hayo ya dini yanaendana na falsafa ya hapa kazi tu.

Mhe. Gambo aliendelea kusisitiza kwamba kutokana na maelekezo hayo ya vitabu vya dini ni wazi kwamba kila mtu anatakiwa kufanya kazi kwa kadiri ya uwezo aliopewa na Muumba ili apate riziki hatua itakayowezesha pia kupunguza wategemezi katika Taifa letu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo RC Gambo kwa niaba ya Rais Magufuli alisisitiza kuwa ni vyema kwa kila mmoja wetu kufanya kazi na kulipa Kodi.

"Kwa yule ambaye hatalipa Kodi ajue kwamba anaikosesha nchi yake mapato ambayo yangeweza kutumika kuendesha shughuli mbalimbali za maendeleo, pia tutambue kwamba huduma zote ni gharama na zinatokana na kodi tunazolipa. 
Hivyo katika Serikali ya Awamu ya Tano asiyefanya kazi na asile na zaidi ya hapo asiyelipa kodi ni vyema akafahamau kwamba analirudisha taifa lake nyuma. Niwaombeni sana viongozi wa Dini muhamasishe waumini walipe kodi kwa mustakabali wa Taifa letu"

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni Mch. Geofrey Mbwana akitoa somo fupi wakati wa maadhimisho hayo alisema amefurahishwa sana na uteuzi wa Mhe. Gambo na ana imani na vijana kwa sababu vijana wakati wao ni sasa na pia ni taifa la leo hivyo wakipewa nafasi kama hii hudhihirisha vipawa vilivyomo ndani yao na bila shaka Mkoa wa Arusha utakua Mkoa kielelezo kwa Taifa hili.

Kanisa hili la Sabato katika Tanzania lilianzishwa Katika kijiji cha Giti kilichopo Mamba Miamba huko Same mnamo mwaka 1903 na kuendelea kukua katika Mji wa Shirati Mara na kisha kufika Arusha na kuanzisha Kanisa la Burka mwaka 1966 likiwa na Jengo moja dogo na waumini nane tu.

Hivi sasa Kanisa hili lina majimbo mawili na waumini zaidi ya 500,000 Tanzania. Kanisa hili pia wanamiliko Chuo Kikuu kimoja, Shule za Sekondari 17, Msingi 11 na shule za awali 11. Pia Kanisa hili lina Hospital moja, Kituo cha Afya kimoja na Zahanati 28.

RC Gambo aliendelea kuwaomba viongozi mbalimbali wa dini wazidi kumuombea na kumtia Moyo Mhe. Rais katika kazi yake ngumu na kubwa anayoifanya kwa maslahi ya Taifa haswa kusaidia wanyonge ambao kwa muda mrefu hawakuwa sehemu ya Agenda kubwa ya Serikali. Pia waendelee kuwasisitiza wanasiasa watambue kuwa wakati wa Siasa  umekwisha ni vyema Mhe. Rais akapewa nafasi ya kuwatumikia watanzania kwa yale aliyoyaahidi kupitia utekelezaji wa ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI na watakutana tena kwenye siasa mwaka 2019 - 2020.

Wednesday, September 14, 2016

Leseni za magari aina ya Noha kuanza kutolewa tena.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (wa katika),kulia kwake akiwa na mwenyekiti wa wamiliki wa magari ya Noha na kushoto ni Mkurugenzi wa SUMATRA,walipotembelea standi ya kuu ya magari Mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,aiagiza Mamlaka ya uthibiti wa usafari wa majini na nchi kavu (SUMATRA) kuendelea kutoa leseni za magari  aina ya Noha kwa Mkoa wa Arusha,hasa kwa yale yanayofanya safari zake kati ya Arusha mjini kuelekea Karatu na Longido.
Aigizo  hilo amelitoa baada yakupata malalamiko kutoka kwa uwongozi wa wamiliki wa magari hayo ukiongozwa na wenyekiti wake Bwana Ally Mkali alisema SUMATRA  wamesitisha utoaji wa leseni za kawaida kwa magari ya Noha na wataanza kutoa leseni  kwa yale yatakayokuwa tayari kutembea umbali wa Kilometa 50 tu.
“Nawaagiza SUMATRA kuendelea kutoa leseni kwa utaratibu uliopo kwasasa na wakati huo mjipange kukutana na wadau wote nakujadili namna yakulitatua swala la magari haya kutembea umbali wa Kilometa 50  hasa kwakuangalia mazingira ya Mkoa wa Arusha nimagumu  na kwakulitekeleza hilo litaongeza gharama kwa wananchi”,alisema Gambo.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo kwa Mkoa wa Arusha Bwana Allen Mwanri, alisema sababu zilizopeleka SUMATRA kupitisha utaratibu huo kwa  magari hayo ni  kutoweza kumudu kutembea umbali mrefu kwani ni hasara napia inahatarisha maisha ya abiria.
“Tuliamua kupendekeza utaratibu huu kwasababu magari mengi ya Noha yalionyesha kushindwa kutembea umbali  mrefu na huku yakibeba abiria zaidi yakiwango kinachoitajika cha watu nane”,alisema Mwanri.
Aidha Mkuu wa kikosi cha usalama barabara Mkoa kamanda Nuru Selemani,amewataka madereva wa magari hayo aina ya Noha kufuata sheria na taratibu za barabarani ilikulinda usalama wao na abiria,na kwakushindwa kufanya hivyo basi sheria zitachukuliwa dhidi yao.
Maamuzi hayo yalitolewa baada ya Mkuu wa Mkoa  na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuwatembelea madereva wa magari hayo maeneo ya standi  kuu ya Mkoa nakujionea hali halisi ya utoaji huduma kwa magari hayo kwani mengi yalikuwa yamesitisha huduma hiyo kwakukosa leseni za usafirishaji.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akiwa pamoja na viongozi wa Mkoa katika kujadili swala la magari ya Noha kutopewa leseni za uwendesheji,katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Tuesday, September 13, 2016

MRADI WAKUKUZA UWEZO WAKUKABILIANA NA ATHARI ZA TABIA NCHI

Mradi wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu.                                                                                                        Kwa Mkoa wa Arusha, mradi huu utawanufaisha wafugaji wa Wilaya tatu za Monduli, Longido na Ngorongoro.   
                           
Lengo la Mradi wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ni kuziwezesha Wilaya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hususani jamii za kifugaji.      
                 
Mradi utawezesha maeneo kame (dry lands) kupata njia mbadala ya ustahimilivu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi katika kuchangia usalama wa chakula na uchumi imara wa wananchi.

Vilevile kuwezesha wana jamii ya kifugaji kupanga mipango yenye kuzingatia matumizi bora ya Rasilimali walizonazo. 

Mambo muhimu yanayozingatiwa katika mipango hiyo ni pamoja na upatikanaji wa maeneo ya malisho na upatikanaji wa maji unaozingatia utawala wa maeneo na usuluhishi wa migogoro juu ya matumizi ya Rasilimali.   

Mradi huu utawezesha  halmashauri hizi tatu kuandaa mipango ya miradi ya maendeleo itakayoweza kukabiliana na athari za tabia nchi katika jamii hizi za wafugaji.

Shirika la Hakikazi Catalyst na Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) yatashirikiana na halmashauri hizi tatu kuwezesha mradi huu kwa halmashauri tatu za Mkoa wa Arusha kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2016 hadi 2021. 

Wednesday, September 7, 2016

WATAKAO HUJUMU MISAADA WATAWAJIBISHWA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amewataka watumishi wote wa Mkoa wa Arusha kutekeleza wajibu wao kama watumishi na kuachana na mambo ya siasa ambayo yanarudisha maendeleo yawananchi nyuma.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro alipofanya ziara ya siku moja Wilayani humo na kukutana na changamoto mbalimbali zikiwepo za migogoro ya ardhi.

Muheshiwa Gambo ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuhakikisha inatatua migogoro yote ya ardhi na ile inayoshindikana kwa ngazi hiyo ndio ipelekwe kwenye ngazi ya Mkoa na yeye atakuwa tayari kuwasaidia.

Aidha ametaka kupewa ripoti ya fedha zinazotolewa na wafadhili katika kila Halmashauri napia zile zinazopelekwa kwa wafugaji zielezwe matumizi yake na yeye atapita kukagua hizo shughuli za maendeleo kwa wananchi ili ajiridhishe na matumizi yake kama ni halali au sio.

Alisema anataka kupata pia taarifa juu ya chakula kinachotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa wananchi wa Wilaya hiyo kama kweli kinawafikia wahusika hususani wananchi wa hali ya chini.

"Ikibainika kuwa fedha za wafadhili na chakula cha msaada vyote vinatumika visivyo basi wahusika wajiandae kuwajibishwa ipasavyo, kwasababu tunatakiwa kuwatendea haki wananchi wetu na sivinginevyo",alisema Gambo.

Aidha aliwaomba wawekezaji wakishirikiana na madiwani waendelee kudumisha uhusiano mzuri baina ya wananchi na wawekezaji hao ili kwa pamoja maendeleo kwa wananchi yapatikane kwa wakati.

Muheshiwa Gambo alikuwa na ziara ya siku moja katika Wilaya ya Ngorongoro kwalengo lakufuatilia shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.

Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo(Hayupo Pichani) alipowatembelea katika ofisi za Wilaya.

Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo atoa ahadi ya ujenzi wa ofisi ya forodha Wilayani Ngorongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,awataka viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro kuchagua eneo maalumu kwaajili ya ujenzi wa ofisi za forodha katika mpaka wa Ngorongoro na nchi ya Kenya.
Ameyasema hayo alipo tembelea eneo la mpaka wa nchi ya Kenya na Tanzania kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro akiambatana na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Bwana. Alphayo Kidata.

"Nawaagiza Viongozi wote wa Wilaya hii kuanzia Mkuu wa Wilaya,Mwenyekiti wa Halmashauri na diwani wa Kijiji cha Njoroi kukaa na wananchi nakisha kuamua ni eneo gani ambalo litafa kujenga ofisi zetu za forodha".

Alisema Serikali ya awamu ya tano ipo karibu sana na wananchi wa hali ya chini hususani katika kuwaletea maendelea hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana kikamilifu na Serikali yao.

Amesema Serikali imeona kuna ulazima wakujenga ofisi za forodha katika Kijiji hicho ili kujipatia mapato kutoka kwa wageni wanaoingia na pia kupunguza uwingizaji wa mifugo kiholela.

Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na Kamishina Mkuu wa TRA katika Wilaya ya Ngorongoro hususani katika Kijiji cha Njoroi ilikuwa na lengo  lakuona ni eneo gani litafaa kuwa na ofisi za forodha ambapo litapunguza uwingiaji wa wageni kutoka nchi jirani ya Kenya ambao wanaingia nchini Tanzania kwalengo lakujipatia mahitaji mbalimbali bila yakutozwa kodi.


Kamishina Mkuu wa Mapato Tanzania(TRA) Bwana Alphayo Kidata,amechangia Milioni Hamsini katika ujenzi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Njoroi  kata ya Ololosokwan. 
 
Pia Kamapuni ya OBC ambao ni wawekezaji wauwindaji katika Wilaya ya Ngorongoro wamechangia pia ujenzi wa Kisima kimoja cha maji katika Kijiji cha Njoroi.

Ujenzi wa Visima hivyo umetokana na baadhi ya wananchi kumuomba Kamishina wa Mapato Tanzania awasaidie upatikanaji wa maji kwasababu wengi wao huwa wanapeleka mifugo yao nchi ya jirani ya Kenya kwaajili yakunyweshea nakuleta usumbufu mkubwa sana kwao.


Baadhi ya wananchi wa kata ya Ololosokwan wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(Hayupo pichani) alipowatembelea katika kata hiyo Wilayani Ngorongoro,Mwanzoni mwa wiki.

Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo pamoja na viongozi mbalimbali wakikagua eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro ambalo litajengwa ofisi za Forodha ilikuongeza mapata kwa Serikali.