Mradi
wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia
nchi unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa Mkoa wa Arusha, mradi huu utawanufaisha wafugaji wa Wilaya tatu za Monduli, Longido na Ngorongoro.
Lengo la
Mradi wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia
nchi ni kuziwezesha Wilaya kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi, hususani jamii za kifugaji.
Mradi utawezesha maeneo kame (dry lands) kupata njia
mbadala ya ustahimilivu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi katika kuchangia usalama wa
chakula na uchumi imara wa wananchi.
Vilevile kuwezesha wana jamii ya kifugaji kupanga mipango yenye kuzingatia matumizi bora ya Rasilimali walizonazo.
Mambo muhimu yanayozingatiwa katika mipango
hiyo ni pamoja na upatikanaji wa maeneo ya malisho na upatikanaji wa maji
unaozingatia utawala wa maeneo na usuluhishi wa migogoro juu ya matumizi ya
Rasilimali.
Mradi huu
utawezesha halmashauri hizi tatu kuandaa mipango ya miradi ya maendeleo
itakayoweza kukabiliana na athari za tabia nchi katika jamii hizi za
wafugaji.
Shirika la Hakikazi Catalyst na Taasisi ya Kimataifa ya
Mazingira na Maendeleo (IIED) yatashirikiana na halmashauri hizi tatu kuwezesha mradi huu kwa halmashauri tatu za Mkoa wa Arusha kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2016 hadi 2021.
0 comments:
Post a Comment