Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,ameongoza mkutano mkuu wa wadau wa utalii wa Mkoa wa Arusha ambao umefanyika katika ukumbi wa AICC Arusha. Ambapo mambo mbalimbali yamejadiliwa kuhusu sekta hii ya utalii na kuangalia jinsi yakuikuza zaidi kwa miaka ya mbeleni.
Akizungumza na wadau hao alisema sekta hii ina changamoto mbalimbali zikiwemo za ongezeko la kodi ya utalii pamoja na kadi nyingine ndogondogo wanazotozwa pindi wakiwa na wageni wao.
“Najua wafanyabiashara wengi hapa wametishika sana nah ii kodi ya utalii ilioanza kutozwa hivi karibuni nakuwafanya muone kuwa biashara zenu zimeanza kuyumba kwa watalii kutotaka kufika tena nchini.”
Alisistiza kuwa kuna fursa mbalimbali katika sekta hii ya utalii ambazo zinaweza kukuza zaidi biashara hii nakuwavutia zaidi wageni kutoka nje napia ushirikishwaji wa wadau wa utalii na Serikali ni kitu chamuhimu sana ndio maana nimeamua kuandaa huu mkutano ili tuweze kuanzimia mambo mbalimbali kwa pamoja.
Akituoa ufafanuzi wa kodi wa utalii iliyoanza kutumika Julai 1,2016 mpaka Agosti 2016 ,Mkuu wa Kitengo cha elimu na mapato Euginia Mkumbo ,amesem kuna ongezeko la kodi kwa kiasi cha bilioni 5.8 ambayo ni asilimia 120 kutoka kwenye kodi za hoteli na utalii wakati mwaka jana ilikuwa bilioni 2.5 kutoka kwenye kodi za hoteli tu.
Aidha ongezeko hilo la kodi ya utalii imeonyesha kunaongezeko kubwa la mapato yaliyoingia Serikalini na wakati huo wageni wengi hawajapatwa na usumbufu wowote tokea kodi hii ya utalii ilipoanza kutumia.
Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators (TATO) bwana Wilbad Chambulo,amesema kuanzishwa kwa kodi hiyo ya utalii kwa upande wao haina shida isipokuwa hawakupewa taarifa mapema na taasisi husika iliwaweze kujipanga.
Kwetu sisi hii kodi haina shida ila tatizo ni taarifa zimetufikia kwa gafla sana nakutufanya tukose mda wakujianda,”alisema Chambulo.
Pia alilisitiza kwa Serikali kusimamia sheria zaidi ili wafanyabiashara wote wa sekta waweze kulipa kodi kuliko kwa sasa ni baadhi yao tu ndio wanalipa na wengine hawalipi.
Aidha aliomba utaratibu wa malipo kwa taasisi husika uwangaliwe upya kwani kwa sasa unamlolongo mrefu sana unaopelekea kuwachukua mda mrefu sana pindi wanapoenda kufanya malipo hayo au kodi zote zingewekwa kwenye fungu moja iliziweze kulipwa kwa mala moja.
Mambo mbalimbali yameathimiwa katika mkutano huo ikiwemo kuimalisha ulinzi na usalama kwa watalii wote watakaoingia mkoani na pia litaanzishwa dawati maalumu lakusikiliza Changamoto mbalimbali zitakazo kuwa zinawakabiri wadau hao wa utalii nakuzitafutia ufumbuzi kwa haraka.
Mwenyekiti wa TATO Wilbad Chambulo akizunguza kwenye mkutano wa wadau wa utalii uliofanyika katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha.
Baadhi ya wadau wa utalii waliohuzulia ukutano wa wadau wa utalii ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa,jijini Arusha.
0 comments:
Post a Comment