Muuguzi Mkuu Mkoa
wa Arusha, Bi. Mwamini Juma Nyakwela, amezindua rasmi mpira wa kiume (Kondom),unaoitwa
ZANA kwa mikoa ya Manyara na Arusha ambayo ipo katika kifungashio
kipya,uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha mafunzo ya afya(CEDHA) Jijini
Arusha.
Uzinduzi huo umefanyika baada ya mipira hiyo kuwekwa
katika vifungashio vipya na hivyo kubadili muonekano uliokuwa umezoeleka zamani.
“Leo hii
tunazindua mipira hii yakiume ambayo imebadilishwa kifungashio lakini ubora
wake uko pale pale,watu endeleeni kuitumia,”amesema.
Watu wengi
waliaacha kutumia mipira hii kwasababu haikuwa kwenye vifungashio vizuri na wakawa
wanatumia aina nyingine ,lakini kwasababu Serikali inawajali wananchi wake
ikaamua kubadili vifungashio ili wananchi waendelee kuzitumia zaidi.
Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa
zilionyesha asilimia 69 ya wanawake na
asilimia 77 ya wanaume wanauelewa mzuri juu ya matumizi sahihi ya mipira ya
kiume lakini ni asilimia 27 tu ndio wametumia mipira hii.
Aidha Kaimu Mkuu wa kitengo cha Elimu,Habari na
Mawasiliano kwa mpango waTaifa wa kudhibiti UKIMWI kutoka Wizara ya
fya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Edda Katikiro,amesema mipira
hii ya jina la ZANA imeshasambazwa rasmi kuanzia Juni 2016 na zilitengenezwa takribani Milioni 21 lakini bado Wizara inaendelea
kutengeneza nyingine zaidi.
Akisisitiza zaidi juu ya mipira hii yenye vifungashio
vipya,amesema wananchi hawanabudi sasa watumie hii mipira kwasababu hakuna
kilichobadilika zaidi ya kifungashio tu, na Serikali inatoa bure kwa nchi
nzima.
“Hii ni ileile mipira ya kiume iliyokuwa inatumika
tokea zamani mabadiliko haya ya vifungashio yasiwaogopeshe watu wakajua ni
mipira mipya,”alisisitiza Edda.
Kutokana na dhana potofu iliyokuwepo katika jamii
juu ya muonekana ambao haukuwa mzuri kwa hii mipira ya kiume hususani huko
nyuma ikapalekea watu wengi kutoziamini kwa ubora wake na hata wengine kutozitumia
kabisa.
Aidha amewata watu wajitaidi kupata elimu sahihi juu
ya matumizi ya mipira hii, ilikupunguza au ikiwezekana kutokomeza kabisa magongwa ya
zinaa,UKIMWI na mimba zisizotarajiwa.
Kwa Mkoa wa Arusha maambukizi ya UKIMWI kwa mwaka
2016 ni asilimia 3.2 kulinganisha ni kiwango cha Taifa cha asilimia 5.1, hivyo
kwa Mkoa kasi ya maambukizi ipo chini,na usambazaji wa mipira ya kiume tayari
Mkoa ulishapeleka maombi yake nakupatiwa mipira hii aina ya ZANA na
imeshasambazwa katika vituo vyote vya afya.
Uzinduzi kama huu umeshafanyika katika mikoa ya
Mbeya na Mwanza na utaendelea zaidi kwa mikoa mingine na juhudi kubwa
imeshawekwa kwa upande wa Serikali katika kuhakikisha mipira hii inatumika kwa
kiasi kikubwa ili kufikia mwaka 2020 UKIMWI uwe umetokomezwa kabisa na wadau
mbalimbali wazidi kushirikiana na Serikali katika mapambano hayo.
|
0 comments:
Post a Comment