Wednesday, September 14, 2016

Leseni za magari aina ya Noha kuanza kutolewa tena.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (wa katika),kulia kwake akiwa na mwenyekiti wa wamiliki wa magari ya Noha na kushoto ni Mkurugenzi wa SUMATRA,walipotembelea standi ya kuu ya magari Mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,aiagiza Mamlaka ya uthibiti wa usafari wa majini na nchi kavu (SUMATRA) kuendelea kutoa leseni za magari  aina ya Noha kwa Mkoa wa Arusha,hasa kwa yale yanayofanya safari zake kati ya Arusha mjini kuelekea Karatu na Longido.
Aigizo  hilo amelitoa baada yakupata malalamiko kutoka kwa uwongozi wa wamiliki wa magari hayo ukiongozwa na wenyekiti wake Bwana Ally Mkali alisema SUMATRA  wamesitisha utoaji wa leseni za kawaida kwa magari ya Noha na wataanza kutoa leseni  kwa yale yatakayokuwa tayari kutembea umbali wa Kilometa 50 tu.
“Nawaagiza SUMATRA kuendelea kutoa leseni kwa utaratibu uliopo kwasasa na wakati huo mjipange kukutana na wadau wote nakujadili namna yakulitatua swala la magari haya kutembea umbali wa Kilometa 50  hasa kwakuangalia mazingira ya Mkoa wa Arusha nimagumu  na kwakulitekeleza hilo litaongeza gharama kwa wananchi”,alisema Gambo.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo kwa Mkoa wa Arusha Bwana Allen Mwanri, alisema sababu zilizopeleka SUMATRA kupitisha utaratibu huo kwa  magari hayo ni  kutoweza kumudu kutembea umbali mrefu kwani ni hasara napia inahatarisha maisha ya abiria.
“Tuliamua kupendekeza utaratibu huu kwasababu magari mengi ya Noha yalionyesha kushindwa kutembea umbali  mrefu na huku yakibeba abiria zaidi yakiwango kinachoitajika cha watu nane”,alisema Mwanri.
Aidha Mkuu wa kikosi cha usalama barabara Mkoa kamanda Nuru Selemani,amewataka madereva wa magari hayo aina ya Noha kufuata sheria na taratibu za barabarani ilikulinda usalama wao na abiria,na kwakushindwa kufanya hivyo basi sheria zitachukuliwa dhidi yao.
Maamuzi hayo yalitolewa baada ya Mkuu wa Mkoa  na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuwatembelea madereva wa magari hayo maeneo ya standi  kuu ya Mkoa nakujionea hali halisi ya utoaji huduma kwa magari hayo kwani mengi yalikuwa yamesitisha huduma hiyo kwakukosa leseni za usafirishaji.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,akiwa pamoja na viongozi wa Mkoa katika kujadili swala la magari ya Noha kutopewa leseni za uwendesheji,katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

0 comments:

Post a Comment