Wednesday, September 7, 2016

Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo atoa ahadi ya ujenzi wa ofisi ya forodha Wilayani Ngorongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,awataka viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro kuchagua eneo maalumu kwaajili ya ujenzi wa ofisi za forodha katika mpaka wa Ngorongoro na nchi ya Kenya.
Ameyasema hayo alipo tembelea eneo la mpaka wa nchi ya Kenya na Tanzania kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro akiambatana na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Bwana. Alphayo Kidata.

"Nawaagiza Viongozi wote wa Wilaya hii kuanzia Mkuu wa Wilaya,Mwenyekiti wa Halmashauri na diwani wa Kijiji cha Njoroi kukaa na wananchi nakisha kuamua ni eneo gani ambalo litafa kujenga ofisi zetu za forodha".

Alisema Serikali ya awamu ya tano ipo karibu sana na wananchi wa hali ya chini hususani katika kuwaletea maendelea hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana kikamilifu na Serikali yao.

Amesema Serikali imeona kuna ulazima wakujenga ofisi za forodha katika Kijiji hicho ili kujipatia mapato kutoka kwa wageni wanaoingia na pia kupunguza uwingizaji wa mifugo kiholela.

Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na Kamishina Mkuu wa TRA katika Wilaya ya Ngorongoro hususani katika Kijiji cha Njoroi ilikuwa na lengo  lakuona ni eneo gani litafaa kuwa na ofisi za forodha ambapo litapunguza uwingiaji wa wageni kutoka nchi jirani ya Kenya ambao wanaingia nchini Tanzania kwalengo lakujipatia mahitaji mbalimbali bila yakutozwa kodi.


Kamishina Mkuu wa Mapato Tanzania(TRA) Bwana Alphayo Kidata,amechangia Milioni Hamsini katika ujenzi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Njoroi  kata ya Ololosokwan. 
 
Pia Kamapuni ya OBC ambao ni wawekezaji wauwindaji katika Wilaya ya Ngorongoro wamechangia pia ujenzi wa Kisima kimoja cha maji katika Kijiji cha Njoroi.

Ujenzi wa Visima hivyo umetokana na baadhi ya wananchi kumuomba Kamishina wa Mapato Tanzania awasaidie upatikanaji wa maji kwasababu wengi wao huwa wanapeleka mifugo yao nchi ya jirani ya Kenya kwaajili yakunyweshea nakuleta usumbufu mkubwa sana kwao.


Baadhi ya wananchi wa kata ya Ololosokwan wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(Hayupo pichani) alipowatembelea katika kata hiyo Wilayani Ngorongoro,Mwanzoni mwa wiki.

Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo pamoja na viongozi mbalimbali wakikagua eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro ambalo litajengwa ofisi za Forodha ilikuongeza mapata kwa Serikali.

0 comments:

Post a Comment