 |
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali na wadau wa sekta ya afya katika uzinduzi wa kampeni ya "Furaha Yangu",Meserani wilayani Monduli.
|
Watakaogundulika wana maambukizi ya virusi vya UKIMWI
wanatakiwa kuwaleta wenza wao wapimwe
pia ili waweze kujitambua na kuishi mda mrefu.
Ameyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo katika uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa virusi vya UKIMWI
kwa hiari ijulikanayo kama “FURA YANGU”.
Gambo amesema bado idadi ya wanaume wanaoenda kupima ni
ndogo sana ukilinganisha na wanawake, hivyo nguvu za uhamasishaji inaitajika
zaidi kwa wanaume.
Ikiwezekana hata kutumia mikusanyika kama sehemu za
ibada na maeneo ya starehe ili kuweza kuwapata wanaume wengi na kuwahamasisha
wajitokeze zaidi.
 |
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu akiwa na (kulia) ni Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Titus Mmasi, wilayani Monduli.
|
Pia wataalamu wanatakiwa kuongeza zaidi wigo wa utoaji
huduma hii kama kutoa ushauri nasaha na kuwahamasisha wagonjwa wapime kwa
hiari.
Akitoa takwimu za hali ya maambukizi kwa mkoa wa Arusha
Mganga mkuu wa mkoa Vivian Wonanji, amesema kwa mwaka 2011/2012 hali ya
maambukizi imeshuka sana kutoka 3.2% hadi 1.9 kwa mwaka 2017/2018.
Amesema hali hii ni nzuri sana kwa mkoa wetu lakini
hatutakiwi kupunguza nguvu hii ya upimaji wa hiari na matumizi ya dawa kwa
wagonjwa kwani mpaka sasa waliogundulika na VVU ni 52.2% wenye umri kati ya
miaka 15-64 ambapo wanaume ni 45.3%na wanawake ni 55.9%.
 |
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta akipata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa Wilaya ya Monduli Dr. Titus Mmasi wakati wa kutembelea mambanda mbalimbali ya upimaji wa kampeni ya Furaha Yangu,Wilayani Monduli.
|
Hali hii inaonesha kuwa bado jitihada inaitajika
kuhamasisha wanaume wajitokeze zaidi katika upimaji na sio upimaji tu hata pia
matumizi ya dawa kwani kati ya wagonjwa 90.9% wanaotumia dawa wanaume ni 86.2%
tu na wanawake ni 92.9%.
Aidha, amesisitiza zaidi hata katika hatua ya kufubaisha
VVU kwa wagonjwa wanaotumia dawa bado msukumo ni mdogo kwa wanaume kwa 84% kati
ya wagonjwa 87.7%.
 |
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta akipima msukumo wa damu (Presha) kama ishara ya uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu, Wilayani Monduli.
|
Kupitia kampeni hii ya Furaha yangu yenye ujumbe wa
Pima,Jitambue,Ishi itasaidia zaidi kuwahamasisha wanaume kupima kwa hiari.
Akitoa takwimu za upimaji katika kampeni hii kuanzia
Agosti 17, 2018 wilayani Monduli mwakilishi kutoka Mkapa Foundation David
Mnkhally amesema,jumla ya watu 5,730 ndio wameweza kupima na 29 ndio
wamegundulika na maambukizi ya VVU.
 |
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta akizungumza na wananchi wa Meserani (Hawapo Pichani) katika uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu,Wilayani Monduli.
|
Ikiwa katika kata ya Monduli Juu jumla ya watu 2.987
wamepima na kati yao wanaume ni 1,206 sawa na 40.3% na wanawake ni 1,781 sawa
na 59.6% na kata ya Meserani waliopima ni 2.743,wanaume ni 1,378 sawa na 50.2%
na wanawake ni 1,365 sawa na 49.7%.
Kampeni hii ya Furaha Yangu ilizinduliwa rasmi mnamo
Juni 2018 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dodoma, na kwa mkoa wa Arusha
zimezinduliwa rasmi Agosti 28, 2018 katika kata ya Meserani wilayani Monduli na
itaendelea katika wilaya ya Ngorongoro.
 |
Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Vivian Wonanji akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya "Furaha Yangu" Wilayani Monduli.
|
 |
Mwakilishi kutoka Taasisi ya Mkapa Foundation David Mnkhally akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni ya "Furaha Yangu",Wilayani Monduli.
|